HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 1, 2024

betPawa yafanya hamshahamsha ya mashabiki wa Mwanza kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, Yamwaga jezi kwa timu mbalimbali

Na Mwandishi wetu

Mwanza. Kampuni ya michezo ya kubashiri ya betPawa imezawadia vifaa vya michezo timu mbalimbali za mkoa wa Mwanza ikiwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya soka na hamsha hamsha ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA kati ya Borussia Dortmund na Real Madrid itakayofanyika Jumamosi, Juni 1, 2024.

Tukio hilo lililopewa jina la Soka Live na betPawa litafanyika eneo la Kona ya Bwiru jijini Mwanza na lilipambwa na hamsha hamsha mbalimbali zikiwemo za mashindano madogo ya kandanda atakayoshirikisha klabu nne za eneo hilo.

Kabla ya mchuano huo, betPawa itatoa msaada wa vifaa vya mpira wa miguu kama jezi na mipira kwa timu ambazo ni Channel Africans FC, Bwiru FC, Majengo FC na Tiger FC.

"Tunaposubiri fainali ya kusisimua ya shindano la kifahari zaidi la Uropa, tunataka pia kurudisha kwa jamii zetu za mpira wa miguu na mashabiki kusaidia kujenga na kukuza michezo nchini Tanzania pia," alisema Meneja Masoko wa BetPawa Borah Ndanyungu.

"Mchezo huu una uwezo wa kutuletea heshima kama nchi na hakuna kinachozuia wanasoka wetu chipukizi kutamani kushiriki katika mashindano hayo mashuhuri," alisema Ndanyungu.

Tukio la Soka Live na betPawa lilifanyika katika Mgahawa wa Juliana jijini Dar es Salaam tarehe Februari 11, 2024 wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Nigeria na wenyeji Ivory Coast.

Katika hafla hiyo, wateja wa betPawa walishiriki challenge mbambali na kujishindia zawadi pamoja na burudani ya muziki mzuri, pamoja na kufurahia fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Kwa fainali ya mwisho ya UCL iliyofanyika Juni 10, 2023 mjini Istanbul, Uturuki, tukio la Soka Live la betPawa lilifanyika Dodoma, likiwakutanisha mamia ya mashabiki wa soka na usiku wa kufurahisha.


Meneja wa Masoko wa kampuni ya betPawa, Borah Ndanyungu akizungumza wakati wa hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa”.


Meneja wa Masoko wa kampuni ya betPawa, Borah Ndanyungu (kulia) akipozi mara baada ya kukabidhi jezi kwa moja ya timu ya Mwanza iliyoshiriki wakati hafla hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa”.

Meneja wa Masoko wa kampuni ya betPawa, Borah Ndanyungu (kulia) akipozi mara baada ya kukabidhi jezi kwa moja ya timu ya Mwanza iliyoshitiki wakati hafla hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa”.



Wachezaji wa moja ya timu wakipozi mara baada ya kukabidhiwa jezi ambazo walitumia katika mashindano maalum ya hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa” mjini Mwanza.



Wachezaji wa moja ya timu wakipozi mara baada ya kukabidhiwa jezi ambazo walitumia katika mashindano maalum ya hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa” mjini Mwanza.


Wacheza shoo wakiburudisha wakati wa hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa” mjini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad