HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 15, 2024

BENKI YA TADB YAAHIDI UDHAMINI MNONO MAONESHO YA WAFUGAJI

Mkurugenzi  Mwendeshaji wa Benki  ya TADB ,Frank.Nyabundangeye  akizungumza katikamaonesho ya wafugaji  yanayofanyika Ubena Zomozi Mkoani Pwani.
Baadhi  ya Wafugaji wakipata maelezo katika banda la Benki ya TADB yanayofanyika Ubena  Zomozi Mkoani Pwani
Kutoka kushoto ni aliyekuwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Alexander Mnyeti  akisalimiana na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki   yaTADB ,Frank Nyabundaye wakati  alipokuaamewasili katika viwanja vya maonesho  hayo ya mifugo Ubena Zomozi, Mkoani Pwani

 

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
BENKI ya Kilimo imeahidi kuwa wadhamini wakubwa na wakuu kadri mtakavyokuwa mnafanya maonesho haya ya wafugaji wa kisasa Tanzania.

Yamesemwa hayo leo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya TADB Frank Nyabundayehe katika ufunguzi wa maonesho ya wafugaji wa kisasa yanayofanyika leo June 14 Ubena Zomozi Mkoani Pwani.

Tumejipanga katika kwa kutoa udhamini mnono kwa wafugaji wa kisasa huku lengo likiwa kupandisha thamani ya mifugo yetu nchini,amesema.

Udhami huu mnono ni kwa ajili ya kuenzi malengo ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan Tanzania ambaye wakati wote amekuwa akisema kuwa wananchi wake wawe wafugaji wa kisasa hivyo tutawawezesha kadri ya uwezo wetu.

Hivyo basi nasema kwamba tumevutiwa sana na haya maonesho na mwaka unaofata pia tutakuwa ndiyo wafadhili wa maonesho haya , nasema maneno machache tu sababu kwa kupitia maonesho haya tumekutanishwa na wafugaji wengi ambapo nichukue fursa hii kuwaeleza kwamba TABD na imekuwa imekuwa ikitoa mchango wake mkubwa katika sekta ya mifugo nchini.

Wiki hii Benki ya kilimo (TADB) imetoa mikopo katika sekta ya ufugaji takribani Mili.25 , kama benki ya serikali pamoja na mambo mengine licha ya kutoa mikopo pia ni jukumu letu kuhakikisha tunaongeza matokeo chanya kwa kila Mtanzania huku jukumu mmoja wapo ni kuhakikisha tunainua kila Mtanzania au kuongeza ajira kwa mtanzania.

"Nitumie fursa hii ndugu mgeni rasmi kutoa tu juu ya mradi ambao tumeanza nao na tumeanza kama 'pilot project, mradi ambao mheshimiwa Raisi anataka kuona vijana wa kitanzania wakipata ajira na maisha bora.

"Tumeanza na huu mradi ambao ni pilot project ambapo tumeweka kiasi cha Mil. 279 kwa ajili ya kuanza na vijana watano na vijana watano hawa tunawasaidia katika sekta ndogo ya maziwa na tumeanza katika mkoa wa Tanga tukishirikiana na Shirika moja linaitwa Solitalidad" amesema Nyabundayehe.

"Dhamira yetu ni kulenga vijana kujikwamua kiuchumi yaani kujiajiri kwa kupitia mradi huu huu, vijana wanapewa mkopo huu ambao tumewapatia kwa riba ya asilimia saba na tunawapatia waweze kulipa kwa miaka saba lakini pia mkopo huu unakwenda kumuwezesha kijana kununua shamba lenye ukubwa wa hekari tano mpaka kumi lakini pia kujenga nyumba ya kuishi na kujenga banda bora kwa ajili ya kufugia ng'ombe kumi na hao ng'ombe kumi wa maziwa tutakaowapatia ndio watakuwa sehemu yao ya kuanzia lakini pia tunawawekea shamba la kuweza kulima malisho na kuweka mfumo wa umwagiliaji katika shamba hilo la malisho na pia kupata vifaa vya kiu kwa ajili ya kushiriki katika ufugaji wa hao ng'ombe" amesema.

Meneja Mwendeshaji wa Benki ya TADB amesema kuwa wapo vijana wengi wa kitanzania ambao unapowaambia ndoto kubwa ya Mhe. Rais juu ya kuwakwamua kiuchumi vijana wa nchi hii wakati mwingine wanakuwa hawajasikia vizuri na hawajaelewa lakini haya mambo yanatokea.

"Hivyo basi nimeona niseme haya hapa ili wale vijana ambao mnataka kufuga na kuingia kwenye kilimo serikali ya awamu ya sita imetuwekeza sisi TADB ambapo naweza nikasema ndiyo mkono wake wa kuume katika kuhakikisha inatoa mikopo katika sekta ya kilimo , ufugaji na kuwapa riba ndogo ya asilimia saba' amesema MkurugenziMwendeshaji wa Benki hiyo.

"Sikusikia vijana wakipiga makofi laiti kama mimi ningelikuwa ni kijana ningeshangilia na kupiga makofi" amesema Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB Nyabundeye.

Ifahamike kwamba nia ya Mhe.Rais ni kuhakikisha kwamba sasa vijana wanapokuwa wamemaliza vyuo wanakwenda wanakaa kwenye mazingira mazuri ndiyo maana tumeweka mifumo mizuri na kuwatengea shamba lenye mifumo ya umwagiliaji na mradi huu tulioanza nayo tunaona kabisa itakuwa ni ya kimkakati na tunaamini vijana wengi sasa watakwenda kufaidika na serikali hii ya awamu ya sita inayowajali vijana na akina mama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad