HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 23, 2024

BALOZI NCHIMBI AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA TIXON NZUNDA SONGWE

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, leo ameongoza maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi na wananchi kutoka maeneo mnalimbali nchini, walioshiriki mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda, yaliyofanyika huko Msinde, Kata ya Mpemba, Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, Jumamosi Juni 22, 2024.

Marehemu Nzunda, ambaye hadi mauti yanamkuta kwa ajali ya gari Juni 18, 2024, akiwa ziara ya kikazi wilayani Hai, alikuwa mtumishi mwandamizi wa Serikali, akiwa amewahi kutumikia nafasi mbalimbali za utumishi wa umma, ikiwemo kuwa katibu mkuu wa wizara mbalimbali, baada ya kupanda ngazi za utumishi wa umma kutokea kuwa Ofisa wa Serikali ngazi ya wilaya.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad