HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 6, 2024

ALIYEKUWA KATIBU MKUU ADC ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI

 

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Aliance for Democtratic Change (ADC) Taifa, Doyo Hassan Doya (katkati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa wa chama hicho baada ya Mwenyekiti wa Sasa Hamad Rashid Mohamed kumaliza muda wake. Kulia  ni katibu wanawake Taifa, Hadija Tabwe na kushto Mwenyekiti wanawake Taifa, Zuwena Abdallah.

Na Mwandishi wetu
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uwenyekiti wa chama hicho, kinachoongozwa na Hamad Rashid.

Doyo amesema hayo leo Juni 6,2024 jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo pamoja na mambo mengine amesema, ameamua kugombea nafasi hiyo kwa sababu anao uzoefu wa kutosha kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho Hamad Rashid Mohamed.

"Mwenyrekiti ameonyesha ukomavu wakulinda katiba ya chama, ambayo imeweka utaratibu wa kiongozi kuongoza kwa vipindi viwili...tunapofuata Katiba za vyama tunaenda kuviimarisha, endapo nitafanikiwa kugombea nafasi hii ntahakikisha naleta mabadiliko makubwa ndani ya chama hasa katika wakati huu ammbao tunaelekea uchaguzi,”amesema.

Amesema, amejipanga kuwa mwenyekiti na kurithi mikoba ya Hamad Rashid, kwani mafunzo yake yamemuimarisha vema.

"Nimepata mafunzo kwake, yeye ni kiongozi mzoefu na mkongwe, elimu niliyoipata kwake kama nikifanikiwa nina mfunzo na uzoefu mkubwa ikiwemo uvumilivu,”amesema Doyo.

Pia Doyo amesema kuwa Juni 11 mwaka huu 2024 atachukua fomu na kuanza kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini 150, Bara 75 na Zanzibar 75 safari ambayo itaanza kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Juni 27 mwaka huu.

Doyo ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwemo mlezi Kanda ya Kaskazini na Mkurgenzi wa Habari amesema kama wanachama watampitisha ataenda kusimamia ajenda ya watu kupata ajira.

“Nitahakikisha pia chama kinaleta ushindani kwenye chaguzi na kupata viongozi watakaosimamia sheria, upatikanaji wa ajira mabadiliko na kusukuma ajenda nyingine za wananchi,”amesema.

Kwa upand3le wake, aliyekuwa mgombea Ubunge Kibaha Mjini katika uchaguzi wa 2020 Scola Kahana ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti akiomba wanachama hao kumuunga mkono.

"Chama nakifahamu sana naomba mapokezi yenu mniunge mkono wananchama na wananchi wote tukashirikiane kuleta mabadiliko,"amesema Kahana.

Naye Mwnyekiti wa vijana wa ADC Ibrahim Pogora amesema ADC kama chama cha siasa sio tamaduni za kawaida mtu anapotangaza nia viongozi wengine kuwepo kwenye tukio hilo ila hiyo inaonyesha kiwa watendaji wanadhamana na Doyo na kitendo cha yeue kuchukua fomu sio cha bahati mbaya.

“Doyo anastahili kuungwa mkono kutokana na historia yake, tunatoa wito kwa wanachama wengine kumuunga mkono kwa kuwa tunadhamana naye,”amesema Pogora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad