HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 27, 2024

WIKI YA MAZINGIRA KUANZA MEI 29, SHUGHULI ZA USAFI, UTUNZJI MAZINGIRA KUFANYIKA

KUELEKEA siku ya Mazingira duniani ambayo hufanyika kila mwaka Juni 5, Tanzania Kuadhimishwa kivingine huku kukiwa na matukio mbalimbali ili kushirikisha wananchi katika usafi na utunzaji wa Mazingira.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Dkt. Selemani Jafo amesema matukio yatakuwa katika kila wilaya na mikoa hapa nchini likiongozwa na tukio la Usafi wa mazingira kwa kila mwanchi kuelekea siku hiyo.

Dkt. Jafo amesema  Juni 5, 2024 ambayo ni kilele kutazinduliwa sera ya Taifa ya uchumi wa buluu ya mwaka 2024, dhana ya uchumi wa buluu inahusisha shughuli za kiuchumi na kijamii zinazotekelezwa katika bahari,Maziwa na mito, mabwawa na maji chini ya Ardhi bila kuathiri mazingira.

Kauli mbiu Mwaka huu ni katika siku ya Mazingira duniani ni “Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahimilivu na Hali ya Jangwa na Ukame.” Kauli mbiu hii inatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua za makusudi kuhimiza matumizi endelevu ya ardhi ikiwa ni moja ya moja ya nguzo muhimu va kutunza na kuboresha mifumo ya ikolojia mbalimbali na ustawi wa viumbe hai, kuongeza upatikanaji wa huduma za kiikolojia ambayo ni muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 na zaidi.

Dkt. Jafo amesema kuwa kutokana na umuhimu wa masuala ya Hifadhi ya Mazingira. Nchi imeendelea kutoa kipaumbele kwa masuala ya hifadhi na usimamizi mazingira katika Nyanja mbalimbali.

Aidha, kutokana na kuwepo kwa changamoto za uharibifu wa ardhi pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi kaulimbiu itakayoongoza maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kitaifa itakuwa ile ile inayoongoza maadhimisho haya Kimataifa.

Amesema maonesho ya mwaka huu yenye lengo la kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa Mazingira yataambatana na matukio mbalimbali yakiwemo Uzinduzi wa mradi wa urejeshaji uoto wa asili unaotekelezwa Wilaya saba katika Mikoa mitano nchini ambayo ni Iringa, Njombe, Rukwa, Mbeya na Katavi.

Matukio hayo yatakuwa kama ifuatavyo;
Mei 31, 2024 Kutafanyika uzinduzi wa kongamano la Mazingiar katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC) ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdori Mpango.

Juni Mosi, 2024 itakuwa ni siku ya kampeni ya usafi nchi nzima ambapo viongozi mbalimbali watakuwepo wakiongoza zoezi hilo kwenye mikoa waliyopangiwa kama ifuatavyo:

Kwa Mkoa wa Dar es salaam kutafanyika usafi wa fukwe wa Coco beach utakaoongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Mpango, Kwa Kanda ya Ziwa Mkoa wa Geita atataongoza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Majaliwa katika HospitalI ya Chato, kwa Kanda ya Kati atakuwa Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Biteko, Nyanda za juu Kusini atakuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Akson, Kanda ya Kaskazini itaongozwa na Jaji Mkuu Tanzania Profesa Ibrahim Juma na wakuu wa Mikoa kwenye mikoa yote nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad