HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 17, 2024

TMA YATOA TAARIFA YA UWEPO WA KIMBUNGA “IALY” BAHARI YA HINDI


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo Mei 7,2024 imesema, mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.

Taarifa hiyo imesema, kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini. Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.

Pia mamlaka imewashauri watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad