HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 18, 2024

Tigo Yatoa Msaada Wa Vitu Mbalimbali Kwa Waathirika Wa Mafuriko Wilayani Karatu

 



KAMPUNI ya Mawasiliano Tigo, imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko Wilayani Karatu

Akizungumza wakati wa utoaji Msaada huo, Meneja mauzo wa Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya ametoa pole kwa wakazi wote wa Karatu lakini pia serikali kwa maafa yaliyowatokea wananchi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao.

“Leo Tigo tupo hapa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu kufuatia maafa ambayo walikumbana nayo ndugu zetu wa Karatu yaliyoathiri maisha ya watu na kukosa maeneo ya kuishi ambapo mpaka sasahivi wanahifadhiwa na ndugu na jamaa, hivyo Tigo kama sehemu ya jamii imeona ni vyema na sisi tushiriki tuwafariji wenzetu kwa chochote “

“Tunakabidhi vitu mbalimbali ambavyo vitaenda kuwasaidia wenzetu kwa muda ambao wamepatwa na tatizo hilo”

“Tumekabidhi magodoro, mablanketi, unga, mchele, maharage na maji ambavyo tunaamini ni vitu ambavyo vinatumiwa kilasiku na vitawasaidia ndugu zetu”

“Tigo tuko pamoja nao na tutaendelea kushirikiana nao kwa namna yoyote” Alisisitiza

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad