HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 22, 2024

TANZANIA YAKABIRIWA NA UPUNGUFU WA LITA BILIONI 9 ZA MAZIWA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

IMEELEZWA kuwa Tanzania ina upungufu wa lita bilioni 9 za maziwa huku uwezo wake wa uzalishaji ni lita bilioni 3.9 kwa mwaka hali hiyo husababisha kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi licha ya kuwa ni nchi ya pili kuwa na mifugo mingi barani Afrika.

Hali hiyo ya uzalishaji wa maziwa nchini imeelezwa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Prof.George Msalya katika warsha ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari jJijini Dar es salaam kuelekea wiki ya maziwa nchini.

Amesema nchi ina ng’ombe zaidi ya milioni 37 lakini wanaofaa kuzalisha maziwa ni milioni 1.3 huku uhitaji wa maziwa ni lita bilioni 12 kwa mwaka hivyo hutumia kiasi kikubwa cha fedha kuagiza bidhaa hiyo ambapo mwaka 2023 shilingi bilioni 23 zilitumika kuagiza lita milioni 11 za maziwa kutoka nje ya nchi.

Aidha amesema kuwa maziwa bora yaliopo nchni ni asilimia 12 ambayo yanaingia katika mfumo rasmi kwa kuyapeleka katika vituo vya kukusanyia maziwa ambavyo vipo vituo takribani 252.

“Maziwa salama ni yale ambavyo yamekusanywa katika vituo vyetu 252 na kwenda viwandani kwa ajili ya kuchakatwa na kupewa namba maalamu na kuyatunza” amesema Prof. Msalya.

Pamoja na hayo amewataka waandishi wa habari kutumia vizuri kalamu zao pamoja na kuyafanyia kazi kwa vitendo yale waliojifuza kwa ajili ya kulisaidia taifa kufahamu zaidi kuhusu tasnia ya maziwa na umuhimu wake.

Amesema kuwa bado wananchi hawana uwelewa mkubwa kuhusu unywaji wa maziwa kwani baadhi ya watu bado wanaamini maziwa kwa ajili ya watoto wadogo.

Mratibu wa mradi shirikishi kati ya wasindikaji na wazalishaji wa maziwa kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB Joseph Mabula amesema mradi huo unatekelezwa katika mikoa 15 Tanzania bara na Zanzibar ili kuongeza uzalishaji na kuhamasisha jamii.

Maadhimisho ya wiki ya maziwa yatafanyika Jijini Mwanza kuanzia Mei 28 hadi Juni Mosi ambayo yataambatana na maoenesho ya shughuli za uwekezaji na ujasiriamali pamoja na kutoa elimu ya uzalishaji,usindikaji na unywaji wa maziwa ili kukuza uchumi na afya za wananchi.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad