HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 24, 2024

SOMO LA USAJILI LA WAMILIKI WA GEREJI LATOLEWA NA TIRA

Kamishna wa Bima Dkt.Baghayo Saqware amewataka wamiliki wa gereji za kutengeneza magari, kujisajili katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ili kuepusha changamoto ikiwemo udanganyifu, ucheleweshwaji wa malipo na huduma mbovu kwa wateja wao ambapo TIRA inawajibika kusimamia haki za pande zote mbili.

Dkt.Baghayo ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa semina ilitolewa kwa wanaotoa huduma za bima nchini, zikiwemo kampuni za Bima na Umoja wa Watengenezaji na Warekebishaji wa vyombo vya moto ili wafuate mwongozo sahihi wa utoaji wa huduma hizo uliotolewa na TIRA.

Pia Kamishna amekubuli ombi la kuwa Mlezi wa Chama cha Wamiliki wa gereji na kuwataka kutanua wigo wa Wanachama kwa kuongeza wanachama hasa mafundi kujiunga katika chama hicho ili na wao wawe na uelewa wa pamoja kuhusu bima.

Nae Mwenyekiti wa muda wa Chama Cha Wamiliki wa Gereji, Hendry Lema, ameiomba TIRA kuweka mazingira rafiki ya usajili na kutoa elimu ili kuwafikia watu wengi zaidi, huku wakipendekeza kuwepo adhabu kwa wamiliki wa gereji ambao watashindwa kufuata miongozo na pia kuwe na fursa sawa za ufanyiaji kazi wa marekebisho au matengenezo ya magari yaliyokatiwa bima.

Meneja Madai kutoka Kampuni ya Bima ya Britam, Neema Mathayo amesema mwongozo huo unatasaidia kumaliza udanganyifu ambao umekuwa ukijitokeza mara Kwa mara katika huduma hizo, huku mwakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), Lugano Mwasomola akisema mwongozo huo utakuwa na msaada mkubwa.

Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki, Zacharia Muyengi amesema mafunzo hayo ni mwendelezo, ambapo pia washiriki wanafundishwa mifumo ya mamlaka na mfumo wa kujisajili, utaratibu wa nyaraka zinazohitajika wakati wa usajili.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad