HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 30, 2024

ROBOTECK LABS Yawaangazia Wabunifu wa MUHAS

  

Abdulwahab Issa kutoka Roboteck Lab  akitoa maelezo wakati alipotembelea banda la MUHAS

KAMPUNI  ya Roboteck Lab imekutana na wabunifu kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili( MUHAS) kwa ajili ya kuwapa elimu juu ya kuwa  na bunifu zinazozingatia kiwango vya kimataifa.

Akizungumza mapema wiki hii katika maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu  jijini Tanga Mtaalam wa Teknolojia ya Tehama kutoka Roboteck  Abdulwahab Issa, amewataka wabunifu kutoka MUHAS kushirikiana na wataalamu wa masuala ya program tumizi ( Applications)   ili kuwasaidia kuwa na bunifu zenye viwango na zinazofuata taratibu za nchi.

“Kampuni yetu inatoa msaada wa kitaaluma kwa anayehitaji tupo tayari kushirikiana katika kuhakikisha bunifu zenu zinafata viwango vya kimataifa”’, amesema. Issa.

Dkt. Nelson Masota, Mratibu wa Ubunifu wa MUHAS

amesema Chuo hicho kikishirikiana na Roboteck kitaandaa mafunzo maalum ya kukuza na kuendeleza bunifu za wasomi wa chuo hicho ili kufikia viwango vya kimataifa.

 "Kurugenzi ya Tafiti, machapisho na Ubunifu ya MUHAS itaisaini mkataba na Roboteck wa kuendesha  mafunzo maalumu yatakayoboresha kazi za wabunifu wetu"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad