HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 26, 2024

Profesa Mkumbo Awapa Kongole Heineken kwa Kutanua Wigo wa Biashara NchiniBaadhi ya Vinjwaji katika picha

Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa vinjwaji vya Kampuni ya Bia ya Heineken. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam Mei 25, 2024 Katik Hoteli ya Serena.

Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade akizungumza wakati wa sherehe za kutambulisha vinjwaji vingine vya kampuni ya HEINEKEN. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam Mei 25, 2024 Katik Hoteli ya Serena.
Meneja wa Masoko na Biashara Lilian Pascal akizungumza wakati wa uzinduzi wa vinjwaji vya Kampuni ya Bia ya Heineken. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam Mei 25, 2024 Katik Hoteli ya Serena.

Baadhi ya watu waliohudhulia katika sherehe za uzinduzi wa Vinjwaji Vya Kampuni ya Heineken.Picha za pamoja


*Asema uwigo wa kuongeza bidhaa kunakwenda kuongeza kodi

WAZIRI wa Uwekezaji na Mipango Profesa Kitila Mkumbo amesema kwa Sekta ya Uwekezaji nchini inazidi kuimarika inayofanya kukua kwa maendeleo ya Uchumi.

Profesa Kitila ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi muunganiko wa kampuni ya Bia ya Heaken na kampuni ya Namibia na kuwa Heaken Beverage itahusishwa vinywaji vya Vileo zaidi ya viwili katika hafla hiyo iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam Mei 25, 2024.

Amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatoa mapato ya kodi ya sh.bilioni 11 sasa wanakwenda kutoa mapato ya kodi ya sh.Bilioni 21.

Amesema kuwa Sekta ya Uwekezaji inavyokua inakwenda sambasamba na kuongezeka kwa ajira nchini pamoja na biashara.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuvutia Uwekezaji na ndio inafanya kampuni za nje kuungana na kampuni zilizopo nchini kwetu kutokana na kuwa mazingira mazuri ya Uwekezaji na biashara.

Profesa Kitila amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mikakati ya Uwekezaji ikiwa ni pamoja wadau wote wanaohusika na Uwekezaji kuwa na sauti moja kwenye eneo kuondoa changamoto kwa wanaotaka kuwekeza nchini.

Profesa Kitila amesema kuwa nchi inakwenda kasi katika Uwekezaji ni pamoja na kuwa na rasilimali watu ya kutosha ambao wanaweza kufanya maeneo mbalimbali.

“Nimefurahi kushuhudia uzinduzi wa Ofisi mpya ya Heineken nchini Tanzania. Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji wa Tanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu na kuongeza ajira. Kujikita kwa Heineken kwenye soko letu ni dhahiri, na ninatazamia kuona matokeo chanya ya jalada lao jipya iliyopanuliwa kwa uchumi na watu wetu.”

Kwa Upande wa Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade, amesema Kuunganishwa kwa biashara ni hatua muhimu katika ukuaji wa kampuni nchini na ni kielelezo ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini upanuzi wa kinywaji cha Heineken zaidi ya kinywaji cha bia.

“Inaonyesha ari yetu kutokana na uzoefu wa kipekee kuhudumia watumiaji wa Kitanzania ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji tukidumisha nyakati za umoja wa kweli. Sasa kuna toleo la kinywaji cha Heineken kwa ajili yako kwa chochote unachohitaji. Uzinduzi huu unaashiria sura ya kuvutia kwetu tunapoendelea kukua na kukidhi soko la Tanzania”. Amesema Fagade

Meneja wa Masoko na Biashara Lilian Pascal amesema kuwa Sekta wanakwenda kuongeza ajira kwani idadi iliyokuwepo ilikuwa ya kinywaji kimoja sasa iko zaidi vinywaji viwili.

Amesema kuwa katika kuongeza ajira wanakwenda kuongeza ulipaji wa kodi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad