HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 2, 2024

NMB yang'ara OSHA!

Benki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta ya fedha na bima kama mshindi wa pili (first runner up) katika tuzo zilizotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa kufunga Wiki ya Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi 2024 yaliyofanyika jijini Arusha.

Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji tuzo alikua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) - Mhe. Deogratius Ndejembi aliyeambatana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi.

Maadhimisho haya hujumuisha shughuli mbali mbali zinazolenga kuendelea kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi hapa nchini. Na benki ya NMB iliweka banda katika viwanja vya ndndndn kuonyesha dhamira na hatua wanazozichukua kuhakikisha wanadhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi katika shughuli zao.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad