HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 14, 2024

NISHATI SAFI ITAWAKWAMUA WANAWAKE KIUCHUMI – SAMIA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Wenyeviti Wenza, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre wa pili kutoka kulia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wa kwanza kulia wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024. Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Kinara wa Nishati Safi ya kupikia, Afrika akishiriki Mkutano huo wa Kimataifa  tarehe 14 Mei, 2024 katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa. Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa akiwa Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afrika. Rais Samia anashiriki Mkutano huo wa Kimataifa tarehe 14 Mei, 2024.Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA) Mhe. Dkt. Fatih Birol pamoja na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa akiwa Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afrika. Rais Samia anashiriki Mkutano huo wa Kimataifa tarehe 14 Mei, 2024.Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA) Mhe. Dkt. Fatih Birol mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa akiwa Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afrika. Rais Samia anashiriki Mkutano huo wa Kimataifa tarehe 14 Mei, 2024.Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA) Mhe. Dkt. Fatih Birol mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa akiwa Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afrika. Rais Samia anashiriki Mkutano huo wa Kimataifa tarehe 14 Mei, 2024.Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema licha ya Afrika kuwa na idadi kubwa ya watu na raslimali zote muhimu, ni bara la chini kuwa na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.

Zaidi ya Waafrika milioni 900 wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia, jambo ambalo linachangia uharibifu wa mazingira, upotevu wa bioanuai na athari za kiafya.

Rais Samia amesema nishati safi ya kupikia ina maeneo matatu. La kwanza hasa maeneo ya vijijini ni uwezo mdogo kutokana na gharama kubwa na upatikanaji wake pia ni tabu.

La pili ni ulimwengu kwa jumla kutolipa suala hilo kipaumbele. Ufadhili mdogo na watu kutokujua fursa za kiuchumi zilizopo kwenye nishati safi ya kupikia inayorejesha nyuma harakati hizo.

Na pia kutokuwepo ushirikiano wa kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa wote. Rais Samia amesistiza upatikanaji, gharama ndogo na suluhu zinazotekelezeka.

Rais Samia pia amesema kuongezeka kwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia itasaidia wanawake kupata fursa zaidi kushiriki shughuli nyingine za kiuchumi, kupunguza umaskini na usawa wa kijinsia.

Licha ya changamoto hizo, Tanzania ina dhamira ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliozinduliwa hivi karibuni uliokusudia kufikia 80% ya Watanzania wanaotumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2034.

Mkutano huu umehudhuriwa na zaidi ya watu 1000 wakiwemo Marais, Viongozi mbalimbali, Asasi za Kiraia, Watu mashuhuri wenye ushawishi kwenye masuala ya nishati safi na wengine wengi.

Malengo hasa ni kuhakikisha mbali na Afrika kupata uelewa lakini pia liwe jambo la Kimataifa ambapo pia itakuwa rahisi kuchangia ili kuweza kutekeleza azma hiyo.

Pia nia ni kuandaa sera madhubuti inayotekelezeka kwa ajili ya nishati safi ya kupikia na kuharakisha ushirikiano wa wadau katika suala hilo.

Inakadiriwa kuwa dola za kimarekani bilioni 4 zinahitajika kila mwaka ili kufanikisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa Waafrika wote ifikapo mwaka 2030.

Mkutano huu umeandaliwa nchini Ufaransa na Shirika la Nishati Duniani (IEA) ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ndio Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad