Na Emmanuel Masaka, Michuzi TV

MWENYEKITI wa Serikali za Mtaa Mbopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam Mohamed Bushir amempongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kutokana na kutoa fedha za Miradi ya maendeleo katika Kata hiyo.
"Kwaniaba ya wananchi wa Kata ya Mbopo tunatoa shukrani za dhati kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ndani ya Tanzania yetu,Mkoa wa Dar es Salaam,Wilaya ya Kinondoni,Kata ya Mabwepande na mtaa wetu wa Mbopo
"Amefanya kazi kubwa mfano Rais ametuletea fedha kwa ajili ya miundombinu ya sekta afya, tayari ujenzi wa hospitali hapa Mbopo umekamilika.Hospitali imeanza kutoa huduma,"amesema.
Pia amesema katika kipindi cha miaka mitano ambacho yeye(Bushir) amechaguliwa na chini ya uongozi wa Rais Samia yamejengwa madarasa katika shule za msingi 10 pamoja na matundu ya vyoo 26
"Hii si kazi ndogo inastahili pongezi kubwa.Pia tumpongeze Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima kwa kubwa anayofanya lakini pia tunaipongeza ofisi ya mtendaji Kata kwa kazi wanayoifanya.
"Mbunge ametusaidia madawati kwani wanafunzi walikuwa wanakaa chini katika Shule ya Msingi Mbopo lakini alifanya ziara katika shule ile na tayari ametatua changamoto ya madawati.Ameshatoa madawati 150 bado 100 ili yafikie 250,"amesema.
Amesema changamoto ni mchakato wa kupima maeneo ili kufanikisha mradi huo,hivyo amewaombe wananchi kushirikiana na Serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa barabara za lami.
Mwenyekiti Bushir amezungumza fedha Sh.milioni 475 ambazo zimetengwa kujengwa daraja la kisasa ambalo litakuwa na uwezo wa kupitisha magari.
Kuhusu huduma ya maji safi na salama, amesema Rais Samia amefanikisha kusambazwa kwa maji ya DAWASA katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mbopo lakini Kuna maeneo mengine bado kunachangamoto ya maji,hivyo ombi la wananchi ni kupatiwa maji maeneo hayo.
"Bado kuna maeneo wananchi wanapata changamoto ya maji , hivyo ni matarajio yetu maji yatakwenda katika maeneo yote yakiwemo ya Chekanao."
Katika sekta ya elimu amesema wanafanya vizuri,wanafunzi wameendelea kufanya vizuri,na watahakikisha wanaendelea kuweka mipango mizuri kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kufaulu huku akisisitiza mwaka Jana shule ya Mbopo imeingia katika shule 10 bora manispaa ya Kinondoni.
"Hivyo niwaeleza wananchi wangu migogoro ya aridhi itaisha kwa suala zima la upimaji na tutakapokamilisha hakutakuwa na migogoro na Mbopo tunataka iwe kama Washington DC ,hivyo lazima aridhi yetu ipimwe na huduma zote za kijamii zinapatikana."
No comments:
Post a Comment