HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 28, 2024

MZUMBE KUFANYA UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA MAONYESHO TANGA

Chuo Kikuu Mzumbe kimewataka wahitimu wa Sekondari na waombaji wengine wanaotaka kujiunga na masomo katika chuo hicho kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada za Umahiri na Shahada za Uzamivu kuchangamkia fursa ya usajili inayotolewa katika Banda la Chuo hicho, kwenye maonesho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal kuanzia Mei 25 hadi Mei 31, 2024 .

Mkuu wa Idara ya Udahili Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt Michael Mangula amesema dirisha la uhadili limeshafunguliwa kwa kozi mbalimbali zinazofundishwa na Chuo Kikuu Mzumbe zikiwemo Masomo ya biashara, sheria , teknolojia ya habari na mawasiliano, Uchumi, Manejimenti utawala, uhasibu ,ujasiliamali , ualimu na, utawala katika afya na nyingine nyingi.

Amesema wananchi wanayo fursa ya kufanya udahili wa hapo kwa hapo kwa njia ya mtandao (online registration) katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu au kufika katika Kampasi za chuo mkoani Morogoro, Mbeya au Dar es salaam Upanga na Tegeta kwa Ndevu kwa mwaka wa masomo 2024/2025 utakaoanza Oktoba mwaka huu.

Aidha Mkuu huyo wa Idara ameongeza kuwa kutokana na kufunguliwa kwa dirisha la udahili, popote mwombaji alipo anaweza kujisajili kwa njia ya mtandao, na kwamba anawasihi waombaji kutembelea tovuti ya chuo ya admission.mzumbe.ac.tz/ au www.mzumbe.ac.tz kwa taarifa zaidi kuhusu kozi na taratibu zingine za kujiunga.

Amewasisitiza wananchi wa jiji la Tanga kuchamkia fursa ya kujiendeleza kielimu kupitia chuo kikuu mzumbe kwani tayari chuo hicho kimepata eneo Wilayani Mkinga kwa jili ya kujenga Kampasi ambapo masomo ya cheti, diploma na shahada za awali yatafundhishwa.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb.) akitazama na kufurahishwa na ubora wa Banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa Maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu
Timu ya washiriki wa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, wanaotoa huduma mbalimbali katika banda la chuo hicho


Wageni mbalimbali waliotembelea maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu wakipata huduma kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Lulu Mussa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliotembelea na kuhudumiwa kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe  wakati wa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akiwa miongoni mwa washiriki wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu. Maadhimisho hayo yalifunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb.)
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za sheria Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Bw. Innocent Mgeta akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu
Mkuu wa kitengo cha ununuzi Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Castor Komba akikabidhiwa zawadi ya kumbukumbu baada ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za kike Ndaki ya Mbeya. Bw. Komba alikabidhiwa zawadi hiyo alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad