HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 28, 2024

MUHIMBILI KINARA UPANDIKIZAJI ULOTO KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA

 

 


Hospitali ya Taifa Muhimbli-Upanga na Mloganzila imeendelea kuandika historia Afrika Mahariki na Kusini mwa Jangwa la Saraha katika matibabu ya ubingwa bobezi kwa Kupandikiza Uloto kwa wagonjwa waliokuwa na saratani ya damu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya Upandikizaji Uloto, zoezi lililoenda sambamba na kuruhusiwa kwa wagonjwa watano ambao wamepata huduma hiyo ambapo kwa sasa imefikisha jumla ya wagonjwa 16 tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2021, idadi inayoifanya Muhimbili kuendelea kuongoza kwa matibabu hayo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Tunapenda kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji uliofanywa wa miundombinu, kusomesha wataalam, ununuzi wa vifaa tiba ambavyo vimewezesha kutoa matibabu haya hapa nchini na kuwapunguzia wananchi gharama za kwenda nje ya nchi kutafuta matibabu ya kibingwa” ameongeza Prof. Janabi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi MNH, Dkt. Mbonea Yonaz amesema huduma ya kupandikiza uloto inatolewa kwa mara ya tatu, kufanikiwa kwa upandikizaji huu kunatoa taswira ya mafanikio na mageuzi makubwa yanayoendelea katika sekta ya afya hapa nchini.

Dkt. Mbonea amebainisha kuwa wataalam wanafurahishwa sana pale wanapofanikisha matibabu ya ubingwa bobezi ikiwemo upandikizaji wa uloto kwa kuwa yanahitaji weledi, dawa na miundombinu wezeshi bora na yenye teknolojia ya kisasa duniani.

Naye, Deogratias Mwolo ambaye ni mmoja kati ya waliopandikizwa Uloto ameipongeza Serikali, uongozi wa hospitali na wataalam kwa kuwezesha kupata matibabu ya kupandikizwa hapa nchini huku wataalam wakitoa huduma bora na nzuri.



 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad