HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 30, 2024

MUHAS Yawe Mstari wa Mbele Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu , Ujuzi na Ubunifu

 

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi wakipata maelezo juu ya kifaa cha ECG mashine kinavyofanya kazi walipotembelea banda la MUHAS katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ujuzi, Elimu na Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga.

Baadhi ya Wanafunzi wa sekondari wakipata maelezo ya program tumizi ( application) ya Afya AI jinsi inayofanya kazi katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ujuzi, Elimu na Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) kimekuwa mstari wa mbele kushiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa kuonesha bunifu zao mbalimbali zilizowavutia wananchi.

Aidha MUHAS imeendelea kuwa kivutio kwa wananchi wanaotembelea banda hilo kwa kuonesha bunifu mbalimbali zilizobuniwa na wahadhiri na wanafunzi kutoka MUHAS.

Maadhimisho hayo yaliyoanza mapema wiki hii yanafanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Popatlal jijini Tanga.

Kati ya Bunifu hizo ni Programu tumizi(Application) inayoitwa AFYA AI ni bunifu iliyobuniwa na mwanafunzi kutoka MUHAS,, Ni App ya simu janja inayotumia teknolojia ya akili mmende ( Artificial Intelligence) kumuwezesha mtumiaji wake kutambua uwezekanao wa kupata magonjwa ya presha na kisukari kisha kupendekeza hatua za kuchukua ili kuepeuka magonjwa hayo pia inamsaidia mtumiaji kujifanyia tathmini ili kujua kuna hatari ya ukubwa kiasi gani ya kupata magonjwa hayo.

Vile vile wabunifu wa chuo hicho wamebuni mfumo wa Mama Care mfumo unaowawezesha watoa wa huduma za afya nchini wenye lengo la kutatua changamoto za uzazi kwa kutumia teknolojia ambayo inahakikisha wanawake wajawazito wanajifungua salama na wanapata ufatiliaji mzuri wakati wa leba.

Pia kuna programu tumizi (application) inayoitwa Pona Health Ni app inayoshughulika masuala mbalimbali ya kiafya ya uzazi , shinikizo la damu, kisukari afya ya akili, na pia ni app inayotoa elimu kuhusu masuala ya ustawi wa jamii.

Wanafunzi wa Muhas wamebuni kifaa kinachotunia teknolojia ya kisasa ya utambuzi wa magonjwa ya moyo – ECG Stereo, MLO HUB ambalo ni jukwaa la kidigitali linalowezesha wauzaji kuthibitisha biashara zao na kuboresha afya ya walaji kwa kutoa ushauri wa lishe bora, Maternal Point of Care ni mfumo wa kidigitali uliokusudiwa kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kuwawezesha wajawazito na watoa huduma katika mchakato wa huduma za afya ya uzazi.

Ubunifu mwingine pia ni AHG Mashine ambayo ni kifaa cha kuzalisha joto kiotomatiki, na bunifu ya Akili Plus ni app inayotoa ushauri wa kitaalamu ili kuimarisha ustawi wao wa kiakili.


Katika maadhimisho haya wananchi wanapata fursa ya kufahamu program mbalimbali zinazotolewa chuoni Pamoja na bidhaa zinazozalishwa chuoni hapo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad