HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 20, 2024

TUNA MKAKATI MAALUM NA COMORO- Prof JANABI

 





Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Prof Mohamed Janabi amesema kuwa wana mkakati maalum wa kutoa huduma za kisada za tiba kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutoka visiwa vya Comoro kutokana na ongezeko la idadi yao katika siku za karibuni.
Prof Janabi alisema hayo alipokuwa akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu aliefika kumuaga.

Prof Janabi ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Utalii wa Matibabu alieleza kuwa kwa hivi sasa wana mratibu maalum wa wagonjwa toka nje ya nchi na pia mkalimani wa lugha ya kifaransa ili kurahisisha mapokezi ya wagonjwa toka Comoro na wako tayari kuwa na kliniki za ufuatiliaji kwenye visiwa hivyo.

“Kwa idadi yao na inavyoongezeka,tunakusudia tuwe na wadi maalum ya wanaotoka Comoro katika siku za karibuni” alisema Prof Janabi.

Kwa upande wake,Balozi Yakubu aliahidi kwenda kufanyia kazi na kuwa na uratibu mzuri wa wananchi wa Comoro kuja nchini kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad