HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 2, 2024

MEI MOSI YAFANA ARUSHA, RC MAKONDA ALIA NA UBOVU WA BARABARA

 
Na. Vero Ignatus Arusha

Maadhimisho ya sherehe za mei mosi kit aifa yamefanyika Mkoani Arusha ambapo yamekuwa na zaidi ya waandamanaji 7000 mbali na wananchi ambao walioshiriki katika maadhimisho hayo.

Akitoa salam za mkoa mkuu mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda aliweza kumuomba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kufikisha salamu kwa Rais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakazi wa Arusha wanatambua mchango wake hasa kwenye sekta ya utalii.

"Wananchi wa jiji la Arusha na mkoa wa Arusha kwa ujumla wake wanayo furaha kubwa sana kwa kazi kubwa aliyoifanya ya 'Royal Tour' na hivi tunaelekea kwenye high season hivyo tunategemea kupata watalii wengi sana, na kwetu sisi wananchi wa kila kada awe ni muuza mchicha, awe ni Bodaboda, awe ni mtu anayelima nyanya, Bilinganya nk anafaidika na utalii kwa kuwa Hoteli zikijaa na yeye anapata nafasi ya kuuza na hatimaye anaendesha maisha yake" Alisema Makonda

Sambamba na salam hizo Makonda aliweza kutoa ombi lake kwa mgeni Rasmi kwamba Rais kwamba jiji hilo Lina mchango makubwa wa wadau wa utalii, hivyo ameomba kusaidiwa kutengeneza barabara ya Jiji hilo,kwani barabara siyo nzuri na wananchi wanashindwa kufanya kazi zao kwa usahihi, lna kwa usalama

"Tunataka kufanya utalii wa Jiji letu kwa lands nzima ya kaskazini tumekubaliana kuanzisha kituo ki moja cha uwekezaji (one stop Center) Jiji la Arusha."

Makamu wa Rais Dkt Philip Isdory Mpango akijibu risala ya TUCTA alisema kuwa kuhusu nyongeza ya mishahara mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilipandisha kima cha chini cha mishahara kwa asilimia 23.3 kutoka shilingi 300,000 (laki tatu) hadi shilingi 370,000 kwa mwezi, lengo la kutoa nyongeza kwa kiwango hicho ilikuwa ni kuwezesha watumishi wenye mishahara ya kima cha chini kumudu gharama za maisha kwa kadri inavyowezekana

Dkt Mpango amesema makundi mengine ya watumishi ambayo yaliguswa na ongezeko hilo la mishahara kwa viwango tofauti kwa kuzingatia ukomo wa bajeti wa mishahara iliyotengwa, huku akiendelea kusema kuwa serikali itaendelea kuhuisha viwango vya mishahara kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi na kibajeti pamoja na ujuzi na utendaji wa waajiriwa, misingi hii ni muhimu ili kuepuka kuchochea mfumuko wa bei kuhatarisha uhimilivu wa deni la Taifa na athari nyingine kwenye uchumi wa Taifa kwa ujumla.

"Haya yote lazima yazingatiwe katika mchakato wa kuongeza mishahara na hususani katika kipindi ambapo uchumi wa Dunia umekumbwa na misukosuko mingi ikiwemo vita baina ya Urusi na Ukraine, vita vya mashariki ya kati inayohusisha Israel, Palestina, Lebanon, Syrian, Iran na Yemen" Alisema Dkt. Mpango

Dkt. Mpango. Amesema Vita hivyo vimepelekea kuvurugika kwa mfumo wa ugavi na kupanda sana kwa bei ya mafuta, mbolea, chuma na chakula, na kama hiyo haitoshi Dunia imekumbwa na majanga mengine ikiwemo mvua kubwa na maporomoko ya udongo ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu, magonjwa na hata vifo.

"Changamoto zote hizi zimeathiri pia uchumi wetu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mama wa Taifa ameniagiza niwaambie wafanyakazi wa Tanzania kuwa endapo hali hii itadumu wafanyakazi wawe na matumaini kwamba atasema jambo hivi karibuni" -Dkt. Mpango

Kawa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kassim Majaliwa amewapongeza wakazi wa Mkoa wa Arusha kwa hamasa na maandalizi ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani leo Mei Mosi, 2024.

Aidha ameahidi kuwa Ofisi Yake itaendelea kishriikiana na vyama hya wafanyakazi kuangalia namna gani wanaweza kutatua changamoto mbakimbali zitakazojitokea.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad