Ahimiza ufungaji wa mita za malipo ya kabla


Amesema kuwa ili kufanikisha utekelezaji wa agizo hilo, Wizara itashirikiana na Mamlaka za Maji Nchini kuhakikisha utekelezaji wa agizo hili unafanyika vizuri.

Ameipongeza Mamlaka kwa kuendelea na utekelezaji mzuri wa majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kuahidi Wizara kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa ili huduma ya majisafi iweze kuwafikia wote sambamba na malengo ya Serikali ya kusambaza maji mijini kwa asilimia 95 na vijijini kwa asilimia 85 kufikia mwaka 2025.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo ameipongeza Serikali kwa jitihada kubwa zinazofanyika za kuhakikisha huduma ya maji inafika kwa kila mwananchi.
"Kazi kubwa imefanyika na Serikali kwa kupitia DAWASA ya kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wote hususani wa Mkoa wa Dar es Salaam," ameeleza Ndugu Mpogolo.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Ndugu Laston Msongole ameishukuru Wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa DAWASA na kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya kutoa huduma ya maji kwa wote.
Amesema DAWASA imejipanga kikamilifu kuhakikisha utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la ufungaji wa mita za malipo kabla linatekelezwa na tayari zoezi limeanza kwa majaribio kwenye baadhi ya maeneo.
No comments:
Post a Comment