HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 19, 2024

WASHINDI 56 MTOKO WA KIBINGWA BETIKA KUSHUHUDIA DERBY DIMBA LA MKAPA KESHO

WASHINDI 56 Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 07 kuitazama Derby ya Kariakoo kati Simba na Yanga itakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa Jijini DaresSalaam.

Akizungumza na Wanahabari mapema Leo Aprili 19,2024 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Tanzania Juvenalius Rugambwa wakati akiwapokea Washindi Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere amesema washindi hao wamepatikana kupitia droo ya mtoko Kibingwa iliyoanza Mapema Februari 2024.

"Kama mnavyowaona hawa ni washindi ambao wamepatikana kupitia kampeni yetu ya mtoko kibingwa,na hawa washindi waliowasili Leo wataenda kuungana na wenzao wa Dar es Salaam nakukamilisha idadi kamili ya washindi 56 na wote watakwenda kulala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano wakifatiwa na bata la Mbagala zakiem kushuhudia burudani ya Muziki wa Bongofleva itakayodondoshwa na chino Wana Man,Mczo,platform, sholo Mwamba na wengine kibao."

.Jevenalius ameongeza kuwa Msimu huu wa mtoko wa kibingwa umekuwa wa kipekee zaidi kwani promosheni yote kulikua na ongezeko la zawadi kwa wki pamoja na mwezi ambapo wametoa zawadi za simu aina ya smartphone pamoja na Android kwa washindi mbalimbali mbali na zawadi kubwa ya kushinda tiketi ya kushuhudia derby yenyewe.

Pia amesema washindi watapelekwa na Ving'ora kwenye kuitazama Deby ya Simba na Yanga na watakaa jukwaa la VIP .

Hata hivyo Jevenalius amesema kampuni ya Betika imekuwa ikitoa ushindi hapo hapo pia itaendelea kuonesha nia yao ya dhati kunyanyua michezo kuanzia mpira wa soko hadi kutoa udhamini katika michezo mbalimbali.

"Kama ambavyo tulivyo sisi mshindi akishinda anapewa zawadi zake hapohapo kwa haraka,tunawaomba watu waendelee kutupia ubashiri kwa kutembelea kwenye website yetu hata hii mechi ya Simba na Yanga ipo hapo"Amesema

Kwa upande wake Balozi wa Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa Baraka Mpenja amesema hii miongoni mwa derby inayowakutanisha watu kutoka Mataifa mbalimbali hivyo kwa washindi hao wanaenda kuandika historia mpya katika maisha yao na ndio dhamira ya Kampuni ya Betika kuhakikisha inawapa nafasi wateja wake .

Aidha amesema anawatakia mchezo mzuri timu zote mbili huku akiwapa moyo washindi hao kuwa watashuhudia mechi hiyo Kifahari zaidi (VIP).

Nao baadhi ya washindi hao,akiwemo Musa John kutoka Mkoa wa Tabora akiwa shabiki wa Simba ameishukuru kampuni ya Betika kupata fursa ya kuitazama Deby ya Kariakoo kwani ilikuwa ndoto yake kuona wachezaji wa timu hiyo.

"Kweli Betika hawana longolongo ,kwa mara ya kwanza nimepanda ndege hata nilipoambiwa nimeshinda sikuamini nilikua Shambani lakini baada ya siku kadhaa kunitafuta kwa mara ya pili na kunijulisha niwatumie vielelezo vyangu ili wanifanyie utaratibu wa safari ya kuja Dar niliamini hivyo nawashukuru sana Betika "

Kutembelea zaidi jinsi ya kubashiri Piga *149*16# au zama www.betika.co.tz.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad