HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 3, 2024

UTEUZI; RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA MAHAKAMA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. Sylvester Joseph Kainda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kainda alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Amemteua Bi. Eva Kiaki Nkya kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bi. Nkya alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Amemteua Bw. Chiganga Mashauri Tengwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Tengwa alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Geita.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad