HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 10, 2024

TRA TEGETA YAWANOA WAFANYABIASHARA

 

Afisa wa TRA kutoka mkoa wa Kikodi Tegeta wilaya ya Kinondoni,.Elinaza Daniel kulia aliyesimama akitoa elimu kwa wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa chama Cha wafanyabiashara, wakulima na wenye Viwanda Wilaya ya Kinondoni,  Martin Gabone akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kupata elimu iliyotolewa na TRA-Tegeta.
Ofisa Usimamizi wa kodi Idara ya Elimu na Mawasiliano Mkoa wa Kikodi Tegeta, Mercy Macha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.





Baadhi ya wafanyabiashara.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara waliosajiliwa katika mfumo wa kodi ya Ongezeko la thamani (VAT)na ambao hawajasajiliwa kutoa kuhakikisha wanatoa risiti halali  ili kupunguza ukwepaji kodi.

Afisa wa TRA kutoka mkoa wa Kikodi Tegeta wilaya ya Kinondoni,.Elinaza Daniel ameyasema hayo leo Aprili 9, 2024 wakati wa semina ya siku moja kwa wafanyabiashara iliofanyika katika ofisi za TRA Tegeta jijini Dar es Salaam 

Amesema, nchi haiwezi kuendelea bila mapato kwani hata miradi inayoendelea kujengwa inatokanana na kodi za wananchi, ninawaomba ninyi wafanyabiashara katoeni elimu hii kwa wananchi wanaoshindwa kudai risiti.

"Hakikisha unatoa risti kila unapouza bidhaa na hakikisha uliemuuzia anachukua risiti liyosahihi na kwa kiwango sahihi alichonunua, risiti sahihi ni Ile yenye namba sahihi ya mlipa kodi(TIN) yako wewe mnunuzi maana unapopewa risiti tayari sisi kama TRA tunakuwa tayari tumekwisha iona kwenye mfumo wetu unaposhindwa kutoa au kudai risiti unasababisha hasara kwa taifa," Amesema Daniel.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama Cha wafanyabiashara, wakulima na wenye Viwanda Wilaya ya Kinondoni,  Martin Gabone amewashuku TRA kwa kuwapa elimu ya kulipa kodi kwani watu wengi walikuwa hawatoi risiti halali kwa wanunuzi wetu kutokana na changamoto za EFD mashine na imani potofu walivyokuwa nayo.

"Tunashukuru kwa kupata elimu hii kwani haijabagua zaidi imeunganisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo ambao wengi  wametoka vyuoni na kuingia kwenye ujasiliamali," amesema Gabone.

"Niwaombe wafanyabiashara wenzangug kuzingatia taratibu zote za kulipa kodi na kutumia mashine husika na kuwataka wafanyabiashara wote  kwenda kutoa elimu hii kwa wananchi ambao hawadai risiti wakati wa manunuzi yao ili liwe kama darasa la mabadiliko na kuachana na ukwepaji kodi kwani unadhoofisha uchumi wa nchi.

Nae Ofisa Usimamizi wa kodi Idara ya Elimu na Mawasiliano Mkoa wa Kikodi Tegeta, Mercy Macha amesema semina hiyo imelenga kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara hao kuhusu ulipaji kodi na juu ya Ongezeko la thamani kwa kufata taratibu zote zilizowekwa ikiwemo kudai risiti, vilevile tumewaelimsha juu ya madhara yatakayowapata endapo watashindwa kufata Sheria hizi.

Amesema kupitia kampeni ya tuwajibike inayoendelea nchini kote Mkoa wa Kikodi Tegeta umefanikiwa kuwafikia wafanyabiashara zaidi ya 200 hivyo mwitikio ni mkubwa na ni mzuri na hii itaendelea  kukuza pato la taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad