HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 17, 2024

POLISI,AMEND WAWAFUNDA MADEREVA BODABODA TANGA

 


Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani limewataka waendesha pikipiki wa watumiaji wa barabara kutumia barabara kwa matumizi sahihi

Akizungumza katika mafunzo yalio andaliwa na shirika la amendi kwa ushirika wa ubalozi wa uswisi mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa tanga wile mwamasika amewataka madereva kusoma na kuhuisha leseni zao ili kuwa na weledi barabarani wanapo kuwa barabarani .


Akitoa elimu katika mafunzo hayo maalumu yalio anadaliwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la usalama barabarani AMENDE kwa ufadhili wa ubalozi wa uswisi katika kata ya Pongwe RTO wille mwamasika amewataka waendesha bodaboda kufuata sheria kuwajali na kusingatia watumiaji wengine wa barabara.

Amesema pamoja na kwamba kuna ajali ambazo haziepukiki ila madereva wanapaswa kuzingatia maelekezo ya matumizi sahihi ya vyombo vyao vya moto kwa kuzingatia watumiaji wengine ikiwemo watembea kwa miguu na wandesha basikeli.

Hata hivyo amewataka waendesha pikipiki kuacha kabisa tabia ya kutumia vilevi wanapo kuwa barabarani kwani ulevi husababisha ajali na kughalimu maisha ya watu ambapo amewataka madereva kufanya matengenezo ya vyombo vyao na kuacha kuingiza vyombo vibovu barabarani.

Katika hatua nyingine Mwamasika amekemea tabia ya bodaboda kubeba watoto zaidi ya mmoja yaani msikaki nyakati za asubuhi wanapo wapeleka shule jambo ambalo ni hatari kwa watoto huku akiwataka bodaboda kuzingatia usafi wanapo kuwa wanatimiza majukum yao.

Amewataka kuzungatia sheria za usalama barabarani wanapo endesha vyombo vya moto kwa kutii alama za barabarani ,kuvaa kofia ngumu .pamoja na kuvaa mavazi yanaweza kuwakinga inapo tokea ajali.

Kwa upande wake Ofisa Miradi kutoka Shirika la Amend Scolarstica Mbilinyi amesema bodaboda zaidi ya 300 wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani kupitia mradi wa vijana wapikipiki unaofadhiliwa na ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania.

Amesema mafunzo kwa waendesha piki piki yanaambatana na ugawaji wa vazi maalum ambalo ni liflecter lita kuwa limebeba ujumbe maalumu wa kujikinga na ajali.

Aidha amesema wanaandaa kanuni za maadili kwa waendesha bodaboda ambazo zita toa muongozo wa utekelezaji wa majukumu isemayo ujanja ni kuwa salama ajali zina epukika

Ally kileo ambaye ni dereva bodaboda kutoka Pongwe amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza umakini wanapo endesha vyombo vyao kwani kabla hawajawahi kupata mafunzo yoyote ya matumizi ya barabara

Amesema awali walikuwa wanaendesha kazi hiyo ya usafirishaji wa abiri bila kuwa na elimu yoyote ya usalama barabarani huku wakiliomba jeshi la police kitengo cha usalama barabarani kuwatambua na kuwapa leseni za udereva ili kurasmisha kazi yao.

Mafunzo hayo ya usalama barabarani yalio andaliwa na shirik la Amend yamehusisha waendesha bodaboda 52 kutoka kata ya Pongwe yakilenga kuongeza weledi na kuwaepusha na ajali za barabarani .













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad