HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 29, 2024

Parimatch yazindua promosheni ya Twenzetu Dubai, Zaylissa, Kiredio waula

 


Na Mwandishi wetu.


Mashabiki wa soka, tenisi, UFC, Kriketi, baseball na michezo mingine sawa wanaweza kushinda tiketi ya kwenda Dubai kwa kubashiri na kampuni ya Parimatch Tanzania.

Pia kampuni hiyo imeingia mkataba na muigizaji nyota, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa kuwa balozi wa chapa yao, “Brand Ambassodor”.

Mbali ya Zaylissa, pia mchekeshaji maarufu nchini, Vincent Njau “Kiredio” naye ametangazwa kuwa balozi chapa wa Parimatch wakiungana na meneja wa habari wa zamani wa Yanga, Haji Manara.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa Parimatch, Levis Paul, jumla ya mashabiki nane (8) watashinda tiketi hiyo kupitia promosheni hiyo ya Twenzetu Dubai na Parimatch ambayo imezinduliwa jana kwenye hotel ya Serena.

Paul alisema kuwa kutakuwa na droo ya kutangaza washindi kila Alhamis na dhumuni kubwa la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kufurahia ushindi.

Alisema kuwa mbali ya zawadi ya kwenda Dubai, pia kutakuwa na bonasi ya Sh5,000 kwa yeyote atakayejisajili na Parimatch na kucheza mchezo pendwa wa Aviator.

“Promosheni hiii ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi kipindi hiki. Lengo kampeni hii ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe za falme za kiarabu huko Dubai.

Kuanzia Aprili 29 mpaka Juni 30, mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wa Aviator ndani ya Parimatch Casino kupitia tovuti yetu www.parimatch.co.tz au App yetu na kadri unavyoweka beti zaidi ndivyo unajiongezea nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda Dubai au kujishindia bonasi ya Sh5,000 kila siku”, alisema Levis.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya ukaribisho ya asilimia 125 hadi kufikia Sh 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao.

Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual.

Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.

Wakati huo huo, Zaylissa amesema amefarijika sana kuwa balozi wa Parimatch na atafanya kazi hiyo kwa bidii zote ili kuleta tija katika kampuni hiyo.“Nawaomba mashabiki zangu wajiunge na Parimatch , kubashiri na kushinda ili kupata nafasi kwenda Dubai,” alisema Zaylissa.
Muigizaji maarufu, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa (kushoto) akionyesha mkataba aliosaini na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch kuwa balozi chapa (Brand Ambassodor). Mbali ya kusainiwa kwa mkataba huo, pia Kampuni ya Parimatch ilizindua promosheni ya Twenzetu Dubai ambayo itapeleka washindi nane watakaobashiri kuitia mchezo wao wa Aviator.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Eric Gelard (kushoto) akisaini mkataba na muingizaji nyota nchini, Zainab Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa kuwa balozi chapa wa kampuni hiyo. Utiaji saini huo ulifanyika sambamba na uzinduzi wa promosheni ya Twenzetu Dubai ambayo washindi nane watapata fursa ya kutembelea nchi hiyo baada ya kubashiri kupitia aviator.
Mkuu wa Masoko wa kamouni ya kubashiri ya Parimatch, Levis Paul akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Twenzetu Dubai ambayo jumla ya mashabiki nane (8) wa michezo watakaoshinda watatembelea nchi hiyo na kukaa kwa muda wa siku nne.

Muigizaji maarufu, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Twenzetu Dubai ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch. Zaylissa ni Balozi Chapa wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Parimatch Tanzania, Levis Paul.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad