HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 30, 2024

ORYX GAS TANZANIA YAKABIDHI MITUNGI YA GESI 100 NA MAJIKO YAKE KWA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI DAR

* wahimizwa kuendelea kuhamasisha wananchi kupitia kalamu zao juu ya umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia ya Oryx na kuachana na nishati chafu

Leandra Gabriel, Na Karama Kenyunko - Dar es Salaam

KATIKA kutimiza dhamira ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuona ifikapo mwaka 2023 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia , Oryx Gas Tanzania imeendeleza juhudi za kufikia malengo hayo kwa kugawa  mitungi ya gesi ya kupikia yenye ujazo wa kilo 15 ipatayo 100 yakiwa na plate mbili kwa wahariri na waandishi wa habari ikiwa ni mwendelezo wa kujenga hamasa zaidi kwa jamii katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia kutoka Oryx Gas.

Akizungumza  wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika leo katika makao makuu ya Oryx Gas, Kigamboni Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Orxy Gas Tanzania Benoit Araman amesema, Oryx Gas Tanzania inatambua umuhimu wa vyombo vya habari kwa jamii na vimekuwa daraja na kiunganishi muhimu katika kufikisha taarifa zinazohusiana na nishati safi ya kupikia hususani gesi ya Oryx.

“Tunafahamu kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na Oryx Gas kwa kutambua umuhimu wa nishati safi tumeibeba kampeni hii kwa vitendo ili kuhakikisha maono ya Rais yanatimia……Lakini tunafungua milango ya kuwahamasisha waandishi wa habari kote nchini kutumia nishati safi ili kufikia lengo la Rais Samia.” Amesema.

Amesema kuwa, Hadi sasa wameshatoa mitungi ya gesi zaidi ya 33,000 katika maeneo mbalimbali nchini na tayari takribani jumla ya shilingi Bilioni 1.5 zimetumika huku kampeni hiyo ikiendelea ili kufikia asilimia 80 ya watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2023.

“Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa makundi mbalimbali wakiwemo Mama na Baba lishe, watumishi wa sekta ya afya na wajasiriamali na tunafurahi kukutana na kundi hili muhimu la waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini tunaamini kupitia kalamu zenu mtahamasisha jamii kwa vitendo katika matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii.” Ameeleza.

Akieleza faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani Oryx Benoit Amesema faida ya nishati safi ya kupikia ni pamoja na kulinda afya za wanawake wanaoathirika kwa moshi unaotokana na mkaa au kuni.

“Moshi utokanao na kuni au mkaa una chembe chembe za sumu ambazo husababisha magonjwa ya pneumonia, cancer ya mapafu na matatizo ya upumuaji…Ni vyema jamii ikafahamu na kuepukana na matumizi ya nishati chafu kwa kupikia” Amefafanua.

Aidha faida nyingine ya matumizi ya nishati
Safi ya kupikia hususani Oryx ni pamoja na kulinda mazingira kwa kutokomeza ukataji wa miti, matumizi ya gesi ya Oryx katika taasisi mbalimbali husaidia kuongeza uzalishaji na kupunguza muda wa taasisi husika kutafuta nishati nyingine ikiweko kuni na mkaa pamoja na kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya wanyama wakali pamoja na kuumia pindi wanapotafuta kuni na kuokoa muda na wanawake kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

Akitoa Elimu ya matumizi sahihi ya gesi ya Oryx Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Oryx, Peter Ndomba amesema wamekuwa wakitoa elimu kabla ya kugawa mitungi na kuendelea kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini hususani vijijini na kutoa elimu tangu mwaka 2021 kupitia programu ya Kijiji kwa Kijiji ili kila Kijiji kiwe na msambazaji walau mmoja na program hiyo imekuwa na kufikia nyumba hadi nyumba.

“Tunafahamu kuwa Tanzania ina nyumba zipatazo milioni 14 na kati ya hizo nyumba milioni 2 zina gesi na sisi lengo letu ni kufikia nyumba milioni nane hadi sita….Kwa sasa tunahakikisha maeneo yanayotumia kuni kwa kiasi kikubwa yanahama na kutumia gesi, na hii ni pamoja  mafunzo ya kulipa kidogo kidogo kupitia ‘Kibubu Polepole’ program ambayo huhamasisha vikundi mbalimbali ikiwemo VICOBA, Mama Lishe, na Upatu ambavyo vimelenga kusaidiana kutenga fedha kwa ajili ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ya Oryx na kufanya matumizi ya gesi kuwa ya kawaida na sio anasa.” Amesema.

Oryx Gas Tanzania yenye makao yake Kigamboni ina hifadhi ya kisasa na salama katika Ukanda wa Afrika Mashariki na ina uwezo wa kusambaza na kutoa Gesi Tanzania bara na Visiwani kwa wakati na muda wowote huku ikiwa ni kituo pekee cha marekebisho ya mitungi ya gesi na kuhudumia nchi mbalimbali za Afrika na kampuni mbalimbali zinazotoa huduma za gesi nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Energies, Benoit Araman, akizungumza na wahariri na waandishi wa habari, kabla ya kukabidhi majiko na mitungi wa gesi ya kupikia, Leo Kigamboni, Dar es Salaam,
 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Energies, Benoit Araman, akiwa katika picha ya pamoja na wahariri na waandishi wa habari, baada ya kukabidhi majiko na mitungi ya gesi ya kupikia, Kigamboni, Dar es Salaam.
 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Energies, Benoit Araman, akikabidhi jiko na mtungi wa gesi kwa mwandishi wa habari wa Michuzi Media, Chalila Kibuda, katika hafla kukabidhi vifaa hivyo kwa wahariri na waandishi wa habari, Kigamboni, Dar es Salaam.
 

Meneja wa Masoko wa Oryx Energies Peter Ndomba akitoa elimu juu ya namna bora ya kutumia gesi safi ya kupikia ya Oryx. Leo jijini Dar es Salaam.



 

Matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
 

Sehemu ya mitungi ya gesi na majiko yaliyotolewa kwa wahariri na waandishi wa habari kutoka Oryx Energies Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad