HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 27, 2024

WAZIRI MKUU APONGEZA JUHUDI ZA TAIFA GAS KATIKA KAMPENI YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI NCHINI, AWAOMBA KULENGA MASHULE

 


WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameiomba Taifa Gas kuhakikisha kwamba inaanzisha mikakati itakayowezesha mashule kuweza kuweka miundo mbinu ya gesi kwa bei nafuu

Akizungumza jijini Dodoma alipotembelea duka la Taifa Gas katika kongamano la wadau wa elimu lililofanyika jijini humo, Majaliwa alitambua juhudi za kampuni ya Taifa Gas katika kampeni ya matumizi ya nishati safi nchini na kusema kwamba ipo haja ya kampeni hii kuelekezwa kwa mashule ili kupunguza matumizi ya Kuni na Mkaa.

Waziri Mkuu aliomba Taifa Gas kuendelea kushirikiana na serikali, ili kupata mwafaka wa shule za Tanzania kupata nishati safi kwa gharama nafuu.

Wiki iliyopita , katika kongamano la kugawa mitaji na Vitendea kazi vya nishati lililofanyika jijini Dodoma, Taifa Gas iligawa mitungi 10,000 iloiyojaa gesi kwa ajili ya watanzania wakaaji wa Dodoma. Mitungi hiyo ilipokeloewa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dr. Phillip Mpango.

Aidha, mapema wiki hii, Taifa Gas ilitangaza kuwa itafungua maduka ya Taifa maarufu kama franchise shops katika kila wilaya ya Mkoa wa Dodoma na vile vile nchi nzima kuwapa akina mama nafasi ya kumiliki mitungi ya gesi na kutumia nishati safi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad