HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 25, 2024

WANYAKYUSA DAR WAIPONGEZA SERIKALI KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI, HUDUMA ZA JAMIII

 

 

Na Mwandishi Wetu

KABILA la Wanyakusya  limeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  kwa kuendelea kuboresha mazingira na maslahi ya watumishi, wakiwemo wazee wastaafu, huduma za kijamii kama afya, elimu na miundombinu ambavyo vimeendelea kuchochea ukuaji wa uchumi.

Pia, Wanyakusya wenye asili ya Mkoa wa Mbeya, wamepongeza jitihada za serikali kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, kuendelea kulinda, kuhamasisha tamaduni za makabila mbalimbali nchini kwa lengo la kulinda maadili kwa jamii.
Wakizungumza Jiji Dar es Salaam na Arch. Elius Mwakalinga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa Kabila la Wanyakyusa wenye asili ya Mkoa wa Mbeya uliolenga kujadili maadhimisho ya utamaduni wao utakaofanyika Mwaka huu.

Mhandisi Mwakalinga amesema kuna umuhimu wa kulinda historia, kutunza kumbukumbu na kuendelea kulinda maadili ya utamaduni wa chimbuko lao na kurithisha kwa watoto wao isipotee vizazi kwa vizazi.

Amefafanua kuwa Mwalimu Nyerere aliwahi kuelezea Taifa lisilo na utamaduni wake limekufa hivyo na wao wasipolinda  utamaduni wao , hakutakuwa kuwa na uhai wa kabila, hivyo nivyema wakaendelea kulinda kupitia maadhimisho hayo.

Wakieleza , kabila la Wanyakusya kwa asili yake ni kabila zuri lenye kuzingatia maadili na utaratibu kwani linazingati mpango mzuri wa mipango miji tangu asili yake ambayo ni kichocheo cha maendeleo kama ambavyo serikali imeendelea kutekeleza na kuhamasisha hilo.

"Tutaendelea kuzingatia suala la mipango ya maendeleo, utafiti na malengo kuendelea kuwa hai na kufanikisha mipango yao mbalimbali ikiwemo maadhimisho yao ya kila mwaka.Kwa asili ni watawala, na watu wa  kudumisha umoja na upendo na kuhamasisha maendeleo kwa jamii."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad