Turaco Collection yashiriki Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB -Berlin yaliyofanyika nchini Ujerumani tarehe 5-7 March 2024.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata akiziwakilisha hotel zao katika maonesho hayo ya ITB- Berlin anasema kwamba, maonesho hayo ni eneo jema kabisa la kujitangaza kubadilishana uzoefu hasa katika dunia ambayo walaji (watumiaji wa huduma) wamekuwa wakibadilika kutokana na mazingira yanayotokea duniani.
Turaco Collection kwa upande wa Dar es Salaam wana Element By Westin Marriott na Delta By Marriott na kwa upande wa utalii wa kaskazini pamoja na bidhaa mbalimbali za utalii pia wana; Ngorongoro Valley Lodge na Manyara View Point Lodge na kwa Zanzibar wana Nungwi Beach Reasort by Turaco, Spice Tree Stone Town by Turaco na Beyt Aly Salaam-By Turaco.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angella Kairuki (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Bw. Florenso Kirambata wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yaliyofanyika nchini Ujerumani hivi karibuni.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh. Hassan Mwamweta (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bw. Damas Mfugale (wa pili kushoto) Meneja Mkuu Nungwi Beach Resort by Turaco (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania Bw. Florenso Kirambata (Kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yaliyofanyika nchini Ujerumani hivi Karibuni.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Bw. Florenso Kirambata (kulia) akiwa na baadhi ya wageni waliofika kwenye banda la Tanzania wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yaliyofanyika nchini Ujerumani hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Bw. Florenso Kirambata katika banda la Tanzania wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yaliyofanyika nchini Ujerumani hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment