HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 29, 2024

SUA YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUDUMISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda akizungumza na wanajumiya wa SUA na viongozi wa dini ya Kiislam.
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Sheikh Jafari Thenei akizungumza na wanajumuiya wa SUA.

Wanajumuiya ya SUA na viongozi mbalimbali wakiwa katika Iftari iliyoandaliwa na chuo hicho.( Picha na Mwandishi wetu, Morogoro).

Na Mwandishi wetu , Morogoro
CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimempongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha amani, upendo na mshikamano kwa watanzania.

Pongezi hizo zimetolewa Machi 28, 2024 na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Raphael Chibunda wakati wa Iftari iliyoandaliwa na SUA kwa wanajumuiya wa dini ya Kiislam wanaofanya kazi chuoni hapo na viongozi mbalimbali wa dini hiyo mkoani Morogoro.

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu hicho amesema umoja, mshikamo na amani iliyopo nchini haitokei hivi hivi, ila ni jitihada za makusudi zinazofanywa na Serikali na ndiyo maana unaweza kuona pamoja na kuwa Iftari imeandaliwa kwa wanajumiya wa chuo lakini maandalizi yake yameshirikisha watu wa imani zote.

“Nitumie fursa hii kumpongeza Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha amani, upendo na mshikamano unaotuweka pamoja katika ushiriki wa mambo mbalimbali” amesema Profesa Chibunda.

Profesa Chibunda amesema Chuo Kikuu hicho kimekuwa na utaratibu wa kuandaa Iftari kwa waumini wa dini ya Kislam kila mwaka wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akitoa salamu za Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Morogoro, mwakilishi wa Sheikh Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Sheikh Jafari Thenei amesema SUA ni chuo cha kuigwa kwani kimekuwa na utaratibu mzuri wa kuwakutanisha waislam na huo ni upendo.

Sheikh Thenei amesema tendo la kuwafuturisha wanajumuiya ya Kiislam chuoni na waumini wa dini hiyo ikiwemo viongozi wa mkoa na wilaya linalofanywa kila mwaka linaendelea kujenga upendo na mshikamo kati ya chuo hicho na waumini wa dini hiyo wa ndani na wa nje.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad