HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 26, 2024

RAIS WA ZANZIBAR AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkaribisha Tende Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, wakati wa hafla ya Iftaar maalum kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja jana 25-3-2024. 

Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika Iftaar maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi , katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakal Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja jana 25-3-2024.

Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika Iftaar maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar iliyofanyika jana 25-3-2024.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftaar maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajini Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar jana 25-3-2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftaar maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar jana 25-3-2024.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad