*Watengeneza faida ya sh.bilioni Mbili kutoa gawio kwa Serikali
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
MFUKO wa SELF (SELF Microfinance Fund) umesema katika kipindi cha kuishia Desemba 31/2023 walitoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 324 kwa wafanyabiashara Wadogo na kati (SME)
Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Self Microfinance Mudith Cheyo amesema kuwa katika mfuko huo umekuwa na mafanikio makubwa katika awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa mfuko huo unaendelea kukua na malengo yake yakitimia katika kuwakomboa watanzania kuweza kupata mikopo nafuu ikilinganisha na sekta nyingine za fedha huku masharti yakiwa ni rahisi ya kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa katika mikopo waliyotoa walikuwa ni kiwango cha mikopo chehefu cha chini ya asilimia 10 na kuweza kujiendesha kwa faida huku wakiwa na wqanufaika 314,055 ambapo kati yao wanawake 166,449 sawa na asilimia 53 na wanaume 147,606 sawa na asilimia 47.
Amesema kuwa mfuko una matawi 12 ambapo mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani wanahudumiwa huku wakiwa wamejiwekea mikakati ya kuongeza huduma za kidjitali katika kurahisisha upatikanaji wa mikopo
Aidha amesema katika kipindi kuishia Desemba 31 mwaka 2023 wameweza kutengeneza faida ya sh.bilioni mbili ambazo wanakwenda kutoa gawio kwa serikali ikiwa ni kurudisha na kuonyesha mfuko unazalisha faida.
Cheyo amesema kuwa fedha za kukopesha sio tatizo milango iko wazi kwa watanzania kupata mikopo na kuweza kufanya kazi za kuzalisha na sio vinginevyo.
Amesema kuwa katika kutoa mikopo hiyo mmoja ya mtanzania amepata kukopa fedha sh.milioni 300 kwa pamoja na ameweza kuendesha biashara huku mmoja akiwa amekopa sh.milioni 100.
Hata hivyo cheyo amesema kuwa wako tayari kufanya kazi na kwenda kasi na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kusukuma maendeleo kwa wananchi kukuza uchumi wa mtu mmoja moja
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Self Mudith Cheyo Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha maofisa wa Mfuko huo na waandishi na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Mfuko wa Self Petro Mataba akitoa maelezo kuhusiana na mfuko huo wakati wa kikao cha Wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri, akizungumza kuhusiana na vikao kazi kati ya Taasisi zilizochini ya Msajili wa Hazina ,jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Mfuko wa Self na wahariri na waandishi wa habari ,jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment