HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 18, 2024

Mashine za Kilimo: Zilizotengenezwa Italia na Zinalenga Kukuza Sekta ya Kilimo Tanzania

 

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Marco Lombardi, (Katikati) akizungumza na wafanyabiashara na wadau wa kilimo wakati wa mkutano ulioandaliwa na Italian Trade Agency kwa kushirikiana na FederUnacoma ambacho ni Chama cha kilimo kutoka Italia mkutano huo umefanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkutano huu amefanyika Machi 18, ukilenga kutoa elimu na ufafanuzi wa mashine za kilimo kutoka nchini Italia kwa wakulima, wasafirishaji, na wataalamu kutoka Tanzania juu ya umuhimu wa teknolojia za kisasa kwenye sekta ya kilimo ulioandaliwa na Italian Trade Agency kushirikiana na FederUnacoma ambacho ni Chama cha kilimo kutoka Italia. Pia Marchi 19 kampuni hizo zitatembelea biashara za ndani ya Tanzania.

Mbali na mkutano huo Kuanzia Aprili 2024, Italian Trade Agency wataanza mchakato wa kuchagua makampuni yatakayolipiwa safari ya kwenda Italia kwa lengo la kujifunza na kuona fursa za kibiashara zinazopatikana nchini humo.

Kampuni za mashine za kilimo kutoka Italia ambazo ni Masscar, Barbieri na Ocmis Irrigazione wamekuja kueleza na kutoa elimu kwa Wakulima na watumiaji wa teknolojia ya mashine za kilimo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na wakionesha dhamira ya kampuni za Italia katika kusaidia ukuaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Washiriki muhimu walikuwa ni pamoja na Balozi wa Italia Marco Lombardi, Fabio Ricci wa FederUnacoma na Riccardo Zucconi, Mkurugenzi wa Italian Trade Agency wa Addis Ababa na wazinduzi wa mkutano wa 46 EIMA.

Pia fursa nyingine muhimu ilikuwa ni kuunganisha wafanyabiashara kwa kuongeza ushirikiano baina yao na ushiriki wa moja kwa moja kati ya makampuni ya Italia na wafanyabiashara wa Tanzania.

Fabio Ricci, Naibu Mkurugenzi wa FederUnacoma, alisisitiza jukumu kubwa kwao na Italia ni kukidhi mahitaji ya teknolojia ya kilimo ya Tanzania. Alisisitiza ongezeko kubwa la uagizaji kutoka Italia lilianza mwaka 2022, akithibitisha kuwa ongezeko la soko na ushawishi unakua kwenye kilimo cha mashine nchini Tanzania.

Maonesho ya kimataifa ya kilimo yamepangwa kufanyika kuanzia Novemba 6 hadi 10 huko Bologna, ikiwa imeandaliwa na FederUnacoma ambapo mkutano huu unatoa jukwaa muhimu kwa ushirikiano kati ya Italia na Tanzania.

Kwa zaidi ya mashine za aina tofauti tofauti 50,000 ikiwa ni mashine na vifaa vya kuonyesha, mkutano huo unatoa suluhisho kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ikiwa ni pamoja na kupanda, ulinzi wa mimea, na mavuno.(Components, Digital,Energy,Green,Idrotech)

Kwa umuhimu maalum ni onyesho la Idrotech, linaloonesha teknolojia za umwagiliaji zenye ubunifu muhimu kwa kuboresha uzalishaji na ustahimilivu wa mazao. Mkutano huo unalenga kuimarisha uchumi wa kilimo nchini Tanzania kwa kukuza maendeleo ya biashara za ndani na kukuza ushirikiano wa kimataifa.

Riccardo Zucconi, Mkurugenzi wa Italian Trade Agency kutoka Addis Ababa na muwakilishi wa Tanzania, amegusia umuhimu wa ushirikiano kati ya Wakala na FederUnacoma.

Wakala ambae amefanya mapinduzi makubwa kutokana na ushirikiano wa kampuni za Italia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Italian Trade Agency na FederUnacoma katika kuhamasisha kilimo cha mashine Italia kimataifa. Alisisitiza mafanikio ya toleo la zamani la EIMA International na kurudia dhamira ya mashirika hayo katika kufanikisha ushirikiano wa kimataifa.

Tukio hili la kimataifa la EIMA Iinalenga ubunifu na ustahimilivu unalingana na kutatua changamoto za kilimo duniani, na kufanya iwe mahali muhimu kwa wadau wa sekta ya kilimo.

Mkutano huo uliofanyika Serena Hotel Dar es Salaam unawakilisha hatua muhimu kuelekea kuimarisha ushirikiano kati ya Italia na Tanzania, na hivyo kufungua njia kwa ushirikiano unaofaidika pande zote katika sekta ya mashine za kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad