HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 6, 2024

LSF na Enabel yaingia makubaliano kusimamia haki za wanawake

SHIRIKA la Msaada ya Kisheria la Legal Services Facility (LSF) na Enabel, shirika la maendeleo la Ubelgiji, wamesaini rasmi mkataba wa ruzuku wa bilioni 10.7 za Kitanzania kutekeleza Maboresho ya Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake kupitia Msaada wa Kisheria.

Chini ya makubaliano hayo LSF na Enabel zitashirikiana kuweka mazingira wezeshi na mazuri ya upatikanaji wa haki kwa kujenga uwezo wa wasaidizi

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng'wanakilala amesema Mradi huo shirikishi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya chini ya mradi unaoitwa "Gender Transformative Action: Breaking the Glass Ceiling" na unalenga kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza usawa katika upatikanaji wa haki hususani kwa wanawake na wasichana.

Ng'wanakilala amesema kupitia mradi huo, LSF itahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zenye ubora zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi ya utoaji haki.

"Tuna furaha kutia saini mkataba huu na Enabel, kwa kuwa umelenga katika kufikia malengo na hatua zote muhimu katika kuboresha upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria hasa kwa wanawake, wasichana, na jamii zote zilizopo nchini Tanzania".

"Kupitia mradi huu, LSF itahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zenye ubora zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi ya utoaji haki. Lulu amefafanua zaidi kuwa mradi huu utaongeza uelewa wa jamii hususani wanawake na wasichana kuhusina na umhimu wa msaada wa kisheria" Alisema Ng'wanakilala

Mwakilishi Mkazi wa Enabel nchini Tanzania, Koenraad Goekint, alisema ushirikiano huo unathibitisha dhamira yao ya kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii iliyo na usawakatika upatakanaji wa haki na inayoshiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria.

"Tunafurahi kuanzisha ushirikiano huu muhimu na Kituo cha Huduma za Kisheria (LSF) wenye nia ya kuimarisha upatikanaji wa haki, hasa kwa wanawake, wasichana, na jamii zilizotengwa nchini Tanzania.

Ushirikiano huu unathibitisha dhamira yetu ya kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii iliyo na usawakatika upatakanaji wa haki na inayoshiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria"

Naye Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania na Afrika Mashariki Christine Grau alisema kupitia mradi huo EU inaendelea kushirikiana na wadau katika kuongeza upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana hasa wale amabo ni whanga wa ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia.
















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad