HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 4, 2024

KITUO CHA AFYA MEDEWELL CHAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUANGAZIA AFYA YA WANAWAKE

 

KATIKAkuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Kituo cha afya cha, Medewell , Mpakani ,Kibaha Mkoani Pwani ,kinatarajia kuwa na kambi maalumu ya ushauri na matibabu ya bure kwa magonjwa ya wanawake.

Kambi hiyo itafanyika kwa siku mbili tarehe 6 na 7 Mwezi Machi mwaka 2024, kituoni hapo Mpakani Kibaha Maili moja kuazia saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.00 alasiri, ambapo akina mama watakaopata kituoni watapatiwa ushauri, matibabu pamoja na kufundishwa namna bora ya kujikinga na maradhi mbalimbali ya wanawake na uzazi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha afya cha Medewell Bashir Khaki, alisema kambi hiyo pia itawahamasisha wanawake kuona umuhimu wa kujitunza na kuweza kufanya maamuzi sahihi juu ya afya zao, kwa ujasili.

“Kama kituo cha afya kinachotoa huduma za afya kwa hisani tunasukumwa na maadili ya kitabibu na tunaamini kuwa ni jukumu letu kutoa matibabu kwa kila mgonjwa bila kujali hali kipato, rangi wala hadhi yake katika jamii"

"Kambi yetu hii ya bure ya ushauri na matibabu ya magonjwa ya wanawake inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wengine wa afya ya mwanamke hapa nchini katika kuboresha huduma za afya ya mwanamke na jamii nzima kwa ujumla"anaeleza Khaki.

Nae Daktari wa Magonjwa ya Wanawake katika kituo hicho, Dkt. Moris Philip Mwanyika, alionya kuwa magonjwa ya wanawake yanaweza kujumuisha masuala mbalimbali, ikiwemo mpangilio mbaya wa siku za mwanamke na maumivi ya tumbo, uvimbe kwenye kizazi , hivyo endapo yakigundulika mapema utapatiwa tiba .

Alifafanua kuwa ,utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya wa mara kwa mara ni muhimu kwa utambuzi wa mapema wa magonjwa mbalimbali ya wanawake na uzazi.

“ Kufika katika vituo vya afya mara kwa mara kwa uchunguzi kunamsaidia mtoa huduma kuweza kumuweka katika uangalizi mgonjwa wake na kuweza kuzuia magonjwa kama vile kansa ya shingo ya kizazi, kansa ya matiti, magonjwa ya zinaa na mengine mengi.

Siku ya Wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ili kutambua mchango na mafanikio ya wanawake kiuchumi, kisiasa na kijamii duniania kote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad