HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 22, 2024

KAMATI YA BUNGE YARIDHIA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU 2024/25

 

 

 

Na: Mwandishi Wetu – DODOMA


 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhia Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.

 

Aidha, Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 21, 2024 bungeni jijini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq ambapo ameipongeza Wizara hiyo kwa kuandaa bajeti ambayo itawezesha utekelezaji wa majukumu sambamba na kuleta mageuzi katika sekta ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

 

Katika kikao hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongozana na Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja kuiongoza menejimenti na Wakuu wa taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kuwasilisha bajeti hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Machi 21, 2024. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Rehema Kipera.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 21 Machi, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akieleza jambo kuhusu utekelezaji wa Mpango na bajeti ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 wakati wa kikao hicho kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 21 Machi, 2024. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja.Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, leo Machi 21, 2024, Bungeni jijini Dodoma.


Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo wakifuatilia maelezo wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, leo Machi 21, 2024, Bungeni jijini Dodoma.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Menejimenti pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo Bungeni, Jijini Dodoma leo Machi 21, 2024 baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kwa Kamati hiyo.

  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad