HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 28, 2024

CHINA KINARA UWEKEZAJI TANZANIA -DKT.TAUS KIDA

 Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, amesema kuwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ya kuhamasisha uwekezaji imefanikisha ongezeko la usajili wa miradi kutoka China kauli ambayo ameitoa wakati wa kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kongamano hilo, Dkt. Kida ameipongeza China kwa mafanikio yake katika uwekezaji katika miaka ya hivi karibuni. Ameeleza kuwa China ni kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza katika kuleta Uwekezaji wa Kigeni (FDI) nchini Tanzania. Kwa mfano, katika kipindi cha Januari 2021 hadi Desemba 2023, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 256 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 2.4 za dola za Kimarekani, katika sekta mbalimbali kama vile viwanda, ujenzi, kilimo, usafirishaji, na huduma.

Dkt. Kida amewahimiza Watanzania kutumia fursa zilizopo katika kushirikiana na wageni ili kunufaika na kupata ujuzi, huku wakiendelea kukua kiuchumi. Amesisitiza kuwa Ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha sekta ya uwekezaji inaendelea kufanya vizuri na kuleta maendeleo kwa manufaa ya kila Mtanzania. Hii ni sehemu ya malengo ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano huo uliofungwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango, ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 ikiwemo kampuni za kibiashara 60 kutoka China na nyingine 240 kutoka Tanzania, lengo likiwa ni kujadili masuala ya biashara na uwekezaji
"Kongamano hili la Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na China limekuja katika muda ambao nchi hizi mbili zinaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi, na katika kipindi hiki chote kimeimairisha mahusiano yao kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mpango wa Belt and Road Initiatives (BRI), huu ni mpango mkubwa wa kidunia unaohusu uboreshaji wa miundombinu ambao uliasisiwa na serikali ya China mwaka 2013 na utatekelezwa katika nchi zaidi ya 150 ikiwemo Tanzania"amesema Dkt. Tausi Kida, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaj
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji  Dkt.Taus Kida akizungumza katika mkutano wa masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akifatilia mada wakati wa Kongamano kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi washiriki wa kongamano la Uwekezaji  kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad