MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 9,2024 ameshuhudia hafla ya kukabidhi rasmi ujenzi wa barabara ya Kimara-Bonyokwa- Kinyerezi yenye takribani Km 8 kwa mkandarasi Nyanza Road Works.
RC Chalamila akiongea wakati wa hafla hiyo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio cha miaka mingi cha wakazi wa Jimbo la Ubungo na Segerea ambao kwa muda mrefu wamekuwa wa kilalamikia ubovu wa barabara hiyo ambayo ilikuwa kikwazo cha maendeleo katika eneo hilo. " Hakika Mhe Rais Dkt Samia ametafuna mfupa ulioshindikana kwa muda mrefu" Alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amemtaka Mkandarasi kujenga barabara hiyo usiku na mchana ili ikiwezekana hata kabla ya mienzi 16 ambayo iko kwenye mkataba iwe imekamilika lakini pia kuhakikisha anazingatia viwango na thamani ya pesa ( value for Money)
Ifahamike kuwa Barabara hiyo ujenzi wake unaanza rasmi kesho Machi 10, 2024 kwa mujibu wa mkandarasi itagharimu kiasi cha pesa za kitanzania zaidi ya bilioni 24 inajengwa kiwango cha lami, mifumo ya maji, daraja, makaravati na kuwekwa taa za barabarani ambapo kukamilika Kwake kutawezesha wakazi wa eneo hilo kufanya Shughuli za kiuchumi saa 24.
No comments:
Post a Comment