HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2024

Wasanii tutumie hifadhi ya Mikumi kwenye kazi zetu-Afande Sele

 

Msanii Nguli nchini Seleman Msindi 'Afande Sele' akizungumza na waandishi habari kuhusiana wasanii kutumia hifadhi ya Mikumi.

 Na Mwandishi Wetu
MSANII Nguli nchini Selemani Msindi 'Afande Sele' amesema umefika wakati kutumia hifadhi ya Mikumi katika matokio mbalimbali katika kupata uhalisia wa maudhui yanayokwenda kwa jamii.

Afande Sele ameyasema hayo Hifadhini Mikumi wakati alipotembelea hifadhi hiyo ,amesema kuwa kwa wasanii wanaofanya filamu wakitaka kuonyesha simba wanafanya uhalisia wake.

Amesema wasanii tutumie hifadhi ya mikumi katika kufanya mabonaza mbalimbali kutokana na kuwa na gharama za chini na kubadili mazingira yaliyozoeleka.

Amesema kuwa licha ya wasanii kutumia hifadhi ya mikumi pia hata watanzania wengine wanaweza kubadili sehemu ya kufurahi na kuona vivutio wakiwa ndani ya hifadhi ya Mikumi.

Hata hivyo ameesema mikumi ni sehemu salama katika kufanya utalii na kuona asili inayoakisi uhalisia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad