HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 27, 2024

Wahitmu AKU nendeni kuonyesha mabadiliko sehemu zenu za kazi -Issa

 

Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia, Omari Issa mahafali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) Dk.Eunice Pallangyo akizungumza baada ya kuahirishwa mahafali katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mhitimu wa Udaktari Bingwa Chuo Kikuu cha Aga Khan Fatma Zahran akizungumza na waandishi habari mara baada ya mahafali hayo kuahiridhwa na kusema haikuwa kazi nyepesi hadi kufikia alipofikia kikubwa ni kumshukuru Mungu
Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia, Omari Issa akiwa katika picha ya pamoja kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia, Omari Issa akiwa katika picha ya pamoja kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya matukio katika picha wakati wa mahafali ya Chuo Kikuu Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
MKUU wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia, Omari Issa amesema wahitimu wa Chuo Kikuu Aga Khan Tanzania (AKU) kwenda kufanya mabadiliko kwa kuonyesha ujuzi katika Taasisi wanazozifanyia kazi

Issa aliyasema hayo katika Mahafali ya Chuo Kikuu Aga Khan cha Wahitimu 67 yaliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Omari alisema vyuo vikuu vya Tanzania lazima vikuze ugavi wa wahudumu wa afya wenye ujuzi kujenga uwezo wa utafiti na uvumbuzi wa nyumbani ili kusaidia nchi kukidhi mahitaji yaliopo.

Amesema mkazo unapaswa kuwekwa kwa kwenye afya ya umma na huduma ya msingi na kuhakikisha huduma za hali ya juu zinapatikana.

"Kubadilisha hali hiyo kutahitaji mafanikio makubwa katika upatikanaji wa elimu pamoja na maendeleo ya mafunzo ya ualimu, mafundisho ya darasani na uongozi wa shule huku tukiendelea kupunguza idadi ya watoto waliopo nje ya shule na kuboresha viwango vya ushindani," amesema.

Kuhusiana na kundi waliohitimu wa 2023 Mhitimu wa Udaktari Bingwa Fatma Zahran alisema "Unapohitimu, unarudi kwenye ulimwengu ambao umejaa changamoto za lakini ndio unakufanya kuonyesha njia katika kukabili changamoto hizo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania(AKU) Dk.Eunice Pallangyo amesema wahitimu wanaokwenda kufanya mabadiliko sehemu zao za kazi kile walichofundishwa kilichokwenda nyakati za mahitaji ya sasa.

Wanafunzi wamehitimu katika vyuo vya Aga khan vilivyopo katika nchi za Afrika Mashariki ambazo Uganda ,Kenya ,Tanzania pamoja nchi ya Pakstan

Amesema kutoa Chuo Kikuu cha Aga Khan katika kozi zao wanatoa kulingana na wanafunzi wanachokihitaji ambapo ndio wanakuwa watu kufanya mabadiliko ya kwenda kutoa huduma bora kwenye jamii.

Pallangyo wamebaini kuwa kufundisha pekee sio suluhisho bali kuona wanaofundishwa masomo wanakwenda kutoa matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa jamii katika kutatua changamoto kutokana na maeneo yao ya kazi.

Amesema kazi ya Wahadhiri ni nyepesi kutokana na kusikiliza zaidi wanafunzi kile wachokuja nacho ambapo wakati wanahitimu matarajio yao yanafikiwa.

"Aga Khan tunajivunia katika kutoa elimu bora inayoendana na mahitaji katika jamii kwenda kutatuliwa changamoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad