HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 22, 2024

UDSM YASAINI MIKATABA YA UJENZI WA MAJENGO NA KUSIMAMIA MAJENGO MANNE KUPITIA MRADI WA HEET

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam kimesaini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET).

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Februari 22, 2024 Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga ambaye amemuwakilisha Waziri Prof. Adolf Mkenda amesema kuanza kwa shughuli za ujenzi ni hatua kubwa na mafanikio ya kujivunia katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa elimu ya juu nchini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

"Ni wazi kuwa kiasi cha fedha ambazo Chuo hiki kimetengewa si kidogo, hivyo Chuo kinatakiwa kuhakikisha kwamba ifikapo Juni 2026 fedha hizi ziwe zimeshatumika kutekeleza malengo ya Mradi". Amesema Mhe. Kipanga.

Amesema kuwa Wizara itaendela kuratibu, kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo. "Tutaendelea kuwahimiza kuongeza kasi ya utekelezaji. Pale mtakapoona mnakwama kwa sababu yoyote ile muwe wepesi kuwasiliana na sisi ili tuona namna nzuri ya kukwamua mchakato".

Aidha ameyataka makampuni yaliyosaini mikataba watambua kuwa ni wajibu wa kisheria na kimaadili wa kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa kadiri ya mkataba. "Tumesema kuwa fedha iliyotolewa kwa ajili ya kazi hii ni kubwa. Ni lazima thamani halisi ya fedha ionekane pale majengo yatakapokabidhiwa. Hili lijidhihirishe pia kwenye ubora wa majengo na kukamilisha ujenzi kwa wakati".

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amesema wamejipanga vizuri kuwasimamia wajenzi na wasimamizi wa ujenzi wahakikishe kuwa tunapata majengo bora na ya kisasa.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema Utekelezaji wa Mradi wa HEET umejikita kwenye kuimarisha na kuboresha miundombinu, ikiwemo ukarabati mkubwa na ujenzi wa majengo mapya pamoja na kufunga vifaa vipya kwenye majengo hayo.

Amesema Chuo kinajipanua na kuwafikia Watanzania zaidi kwa kuanzisha kampasi mpya katika mikoa ya Lindi na Kagera katika fani za Kilimo na Biashara.

Hata hivyo amesema kuwa ili kuendana na matumizi ya TEHAMA, Chuo kimejipanga kuimarisha miundombinu ya TEHAMA ili kuboresha ufundishaji na utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo ulinzi na usalama. Matumizi ya TEHAMA yatapewa msisitizo mkubwa kwenye kufundisha na kujifunza.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye (kushoto) akiwa na mmoja wa Kampuni ya ujenzi wakisaini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET).Hafla hiyo imefanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye (kushoto) akiwa na mmoja wa Kampuni ya ujenzi wakionesha mikataba waliosaini kwaajili ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET). Hafla hiyo imefanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET) iliyofanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET) iliyofanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET) iliyofanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET UDSM, Prof. Bernadeta Killian akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET) iliyofanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET) iliyofanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET UDSM, Prof. Bernadeta Killian wakiwa kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET).Hafla hiyo imefanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET).Hafla hiyo imefanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
Meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi katika elimu ya Juu (HEET).Hafla hiyo imefanyika leo Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad