HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2024

UDSM YAINGIA MKATABA WA MAREJEO NA KAMPUNI YA SEACOM KUBORESHA HUDUMA YA INTERNET CHUONI

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeingia mkataba wa marejeo na Kampuni ya SEACOM kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti Chuoni.

Katika marejeo hayo ya kimkataba, UDSM imefanikiwa kuongeza uwezo wa intaneti itakayopatiwa na SEACOM kutoka Megabaits 155 kwa sekunde (STM 1) hadi kufikia Gigabaits 10 kwa sekunde (STM 64).

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Februari 8,2024, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema kuwa Chuo kina Mpango Kabambe wa miaka 10 wa TEHAMA (UDSM ICT Master Plan) ambao ulipitishwa na Baraza la Chuo.

"Intaneti yenye kasi kubwa itakayopatikana kupitia mkataba huu, itawezesha utekelezaji wa Mpango huo. Kwa ujumla, kupitia Mkataba huu, tutakuwa na mtandao wenye kasi zaidi utakaokiwezesha Chuo kujiimarisha katika shughuli za taaluma na huduma kwa jamii". Amesema

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala Bernadetha Kilian amesema kuwa baada ya kuboresha miundombinu husika, huduma hiyo itapatikana katika Kampasi zote za Chuo na zile zilizo nje ya Dar es Salaam kama vile IMS (Zanzibar), MRI (Dodoma na Nzega), MCHAS (Mbeya) na Kampasi mbili mpya za Lindi na Kagera.

"Kwa kutumia uwezo huo wa Intaneti yenye kasi kubwa, UDSM itaweza kutekeleza dhamira yake ya kuwa KAMPASI MAIZI “SMART CAMPUS” ambapo shughuli muhimu za Chuo zinatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao". Amesema

Aidha amesema kuwa kupitia huduma hiyo, wanatarajia ufanisi wa Chuo katika Ufundishaji (Teaching), Utafiti (Research) na Huduma kwa Umma (Public Services) utaongezeka.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Seacom (TZ) LTD Bw. Joe Vipond amesema kuwa wameamua kuingia mkataba huo ili kuendelea kuboresha huduma ya internet yenye nguvu zaidi ya mwanzo.

Amesema wataendelea kushirikiana na uongozi wa Chuo katika kuondoa changamoto ya internet kwenye maeneo ya Chuo hicho pamoja na Kampasa zote zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Seacom (TZ) LTD Bw. Joe Vipond wakisaini mkataba wa marejeo kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Seacom (TZ) LTD Bw. Joe Vipond wakionesha mkataba waliosaini wa marejeo kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Seacom (TZ) LTD Bw. Joe Vipond wakibadilishana mkataba wa marejeo kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa marejeo kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Seacom (TZ) LTD Bw. Joe Vipond akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa marejeo kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala Bernadetha Kilian akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa marejeo kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma ya Intaneti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 8,2024 Jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad