HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 19, 2024

SILAA AKABIDHI MAGARI YENYE THAMANI YA BIL.2.7 MRADI WA UBORESHAJI MILKI ZA ARDHI NCHINI

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa mapema leo amekabidhi magari 16 yenye thamani takriban Bil. 2.7 za Tanzania zitakazotumiwa na Mradi wa Usalama wa Uboreshaji wa Milki za Ardhi Nchini ambazo ni sehemu ya magari mengine kama hayo 54 yatayowasilishwa baadae ikiwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi huo.

Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya makabidhiano hayo Waziri Silaa ameweka wazi kuhusu matumizi sahii ya magari hayo ikiwemo kuyatunza na kuyafanyia matengenezo kwa wakati ili utekelezaji wa mradi huo uweze kutekelezeka kama ilivyopangwa.

‘’Waziri Silaa ameonya watumiaji wa magari hiyo kuzingatia weledi wa kazi yao na kuyatumia kama inavyotakiwa akiongeza kuwa magari hayo yasuije yakatumika kufanya mambo mengine ikiwemo kubeba mikaa au kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo harusi.

‘’Magari haya yatumike kwa kazi za mradi wale wote watakao kabidhiwa magari haya wayatumie vizuri, wayatunze tusione magari haya yamebeba mkaa au kufanyika katika shughuli za harusi tungependa kuyaona yakifanya kazi ya Mradi tunaamini magari haya yanaenda kuongeza kasi na chachu ya utekelezaji wa mradi’’. Waziri silaa aliongeza.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga wakati akimkaribisha Waziri huyo kukabidhi magari hayo amesema thamani ya gari moja ni takribani Mil. 129.9 za Tanzania na magari hayo ni sehemu ya magari 70 yatakayonunuliwa kwa msaada wa Benki ya Dunia.

Eng. Anthony Sanga amesema mradi huo mkubwa wa Benki ya Dunia thamani ya Bil. ni 300 na utakelezaji wake unaendelea katika Halmashauri mbalimbali hapa Nchini hivyo matumizi ya magari hayo yatapelekwa katika baadhi ya Halmashauri ili kuendeleza shughuli za mradi huo.

Kwa Upande wa Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph I.Shewiyo amesema uwepo wa magari hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa utekezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu kuu nnne ambazo ni Usalama wa Milki, uimarishaji mifumo ya taarifa za Ardhi na ujenzi wa miundombinu ya Ardhi.

Hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa magari ya mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki za ardhi yamefanyika makao makuu ya ofisi za Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mtumba jijini Dodoma na kushuhudiwa na viongozi na watumishi mbalilimbali wa Wizara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa akikata utepe kukabidhi magari mapya kwa aijili ya Mradi wa Uboresweshaji wa Milki za Ardhi Nchini.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa akikabidhi ufungua wa gari mpya Katibu Mkuu Anthony Sanga kama ishara ya kuanza kutumika kwa magari hayo kwenye Mradi wa Ubore sweshaji wa Milki za Ardhi Nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad