HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 29, 2024

SAMSUNG YAJIVUNIA MAUZO YA TV ZAKE

 

Kwa mujibu wa utafiti wa masoko uliofanywa na -OMDIA imeitaja kampuni ya Samsung electronics Tanzania kukua kwa asilimia 30.1 kwa uuzwaji wa runinga katika soko la kimataifa kwa mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics Tanzania Manish Jangra huku mafanikio hayo yakichangiwa na mikakati iliyoweka na kampuni hiyo katika kuleta runinga hizo kwa watanzania.

Amesema kampuni hiyo imevuka mauzo ya jumla na kufikia runinga milioni 40 huku safu ya runinga za QLED kwa mwaka jana pekee yalifikia mauzo milioni 8.31.

Tangu kuzinduliwa kwake 2017 kampuni hiyo kupitia bidhaa zake imeonekana kuchangia pato la Taifa hasa katika ulipaji kodi.

Aidha katika kuadhimisha mfululizo wa miaka 18 ya kampuni hiyo imeendelea kuleta vifaa bunifu ikiwemo runinga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad