HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 24, 2024

SAMSUNG, TIGO WAZINDUA SAMSUN GALAXY S24

 Na Mwandishi wetu
UTAFITI uliofanywa na chama cha waendesha huduma ya simu za mkononi Tanzania -TAMNOA, imeonesha kuwa mwaka 2019 mapato ya soko la simu yalikadiriwa kufikia shilingi trillioni 2.7 sawa na asilimia 1.9 ya pato la Taifa.

Katika kuunga mkono jitihada hizo kampuni ya Samsung electronics Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Tigo imezindua simu lengo ni kuongeza chachu katika uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa jumla ikiwemo sekta ya biashara, kilimo, uvuvi na mifugo.

Akizungumza muda mfupi baada ya uzinduzi wa ushirikiano huo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini Henry Kinabo amesema tangu mwaka 2022 Tigo imewekeza zaidi ya shilingi trillioni moja huku fedha hizo zikielekezwa katika kutanua wigo maboresho ya 5G ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

"Ushirikiano wetu Tigo na Samsung katika kutambulisha simu ya Galaxy S24 una thibitisha dhamira yetu ya kutoa vifaa vya hali ya juu kwa wateja wetu kwa jumuisha wa mtandao wa 4G na 5G" Amesema Kinabo.

Manishi Jangra ni Kiongozi wa biashara Kampuni ya Samsung electronics Tanzania amesema kuzinduliwa kwa simu mbalimbali ikiwemo Galaxy S24 ni hatua mihumi katika kukuza uchumi kupitia simu janja.

"Ujio wa Samsung Galaxy S24 umepokelewa vizuri na wateja wetu huku ongezeko la oda likiendelea kuongeza mara mbili ya mwanzo kwani asilimia 69 ya watumiaji wameonekana kuchagua simu hii" Amebainisha Jangra.

Itakumbukwa kuwa ripoti ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania -TCRA kwa robo ya nne mwaka 2023 iliitaja kampuni ya Tigo kuongoza kwa ubora wa huduma hivyo ushirikiano na Samsung utasaidia kuleta ujumuishi sekta ya mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad