HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 16, 2024

Nusu ya Waandishi wa Habari Nchini Tanzania Wameripoti Kutishwa, Kunyanyaswa Wakiwa kazini

 



* Maafisa wa Serikali watajwa kuwa ni chanzo kikuu cha Vitisho

*Waandishi wengi wa habari hawana ajira za Kudumu

ASILIMIA 50 ya waandishi wa habari nchini Tanzania wameripoti kukumbana na vitisho, manyanyaso, mateso au kushambuliwa katika kazi zao. Wawili kati ya kumi 22% wamekamatwa au kuzuiliwa na mamlaka,. na idadi sawa na hiyo wamekumbana na unyanyasaji wa kijinsia 20% au kunyang'anywa vifaa vyao vya kazi (20%).

Hayo yamesemwa leo Februari 15, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa wa taasisi ya utafiti ya Twaweza, Aidan Eyakuze wakati akiwasilisha Matokeo ya Utafiti uliofanyika kwa Septemba hadi Novemba 2023 juu ya Uzoefu na Maoni wa Waandishi wa Habari wa Tanzania.

Amesema kuwa utafiti huo umefanywa na Twaweza ikishirikiana na MISA-TAN, Jamii Forums, UTPC na TAMWA.

Wametoa matokeo hayo kwenye jarida la utafiti lenye kichwa cha habari Sauti za Waandishi katika Uzoefu na maoni ya waandishi wa habari wa Tanzania.

Jarida hilo linawasilisha takwimu kuhusu uzoefu na maoni ya waandishi wa habari wa Tanzania.

Maoni yalikusanywa kutoka kwa kwa wanahabari 1,202 wakiwemo waandishi wa habari, wahariri na wanablogu.

Wanahabari hawa wamepatikana kutokana na kanzidata za uanachama wa vyama mbalimbali vya vyombo vya habari ambavyoni Chama cha Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC),

Chama cha Wanawake Waandishi wa Habari Tanzania (TAMVWA), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-Tan) na Jamii Forums.

Amesema Mahojiano yalifanyika kwa njia ya simu kati ya Septemba 23 na Novemba 7, 2023.

Utafiti huo umeonesha kuwa Waandishi wengi wa habari wana ajira zisizo za kudumu na zisizo za uhakika. Wawili kati ya kumi 20% wanataja kuwa ajira zao ni za kudumu, ikilinganishwa na sita kati ya kumi 60% wanaosema ni za muda na wawili kati ya kumi 18% wanaosema wanaitwa kazini pale tu wanapohitajika.

Nusu 50% wanayo mikataba iliyosainiwa. Waandishi wengi wa habari 63% wanasema ni vigumu kujipatia kipato kinachokidhi mahitaji muhimu kupitia uandishi wa habari, wakati wachache 5% wanasema si tatizo.

Mmoja kati ya waandishi watatu 36% wana kazi nyingine inayowalipa mbali na kazi yao ya uandishi. Ni wanahabari wawili kati ya kumi 19% tu ndio wangependelea watoto wao wafuate nyayo zao kuwa waandishi wa habari.

Uzoefu wa waandishi wa habari kuhusu hatari wakiwa kazini ni mkubwa. Nusu 50% wanaripoti kwamba wamewahi kutishiwa, kuteswa au kushambuliwa wakiwa kazini. Waandishi wa habari kwa kiasi kikubwa wanawatuhumu maafisa wa serikali kama chanzo kikuu cha vitisho; zaidi ya nusu 56% wanasema maafisa wa serikali ni chanzo kikuu cha vitisho, zaidi ya kundi lingine lolote.

Wanahabari walio wengi 86% wanasema rushwa ipo katika sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na 36% wanaosema rushwa ipo kwa kiwango kikubwa. Aina za rushwa zilizokithiri ni malipo kwa ajili ya kuchapisha 55% au kutokuchapisha 53% habari fulani. Karibu wote (956) wanasema wanakubali pesa kutoka kwa watu au taasisi zinazohusika na Habari, 23% wanakubali mara kwa mara, na 72% wameshakubali mara kadhaa.

Mmoja kati ya kumi 10% anaripoti kupokea 'mara zote' zawadi au pesa ili kubadilisha maudhui, na nusu 53% wanasema wameshafanya hivyo angalau mara moja.

Aidha, waandishi wa habari wanahisi kwamba vyombo vya habari nchini Tanzania vina uhuru mdogo wa kufanya kazi bila kudhibitiwa au kuingiliwa. Wanahabari sita kati ya kumi hawajisiki huru kuripoti kuhusu rushwa 60% au masuala yanayohusiana na vyombo vya ulinzi na usalama 61%

"Waandishi wa Habari wana majukumu muhimu sana nchini, yakiwemo kuwataarifu, kuwaelimisha na kuwaburudisha wananchi, pamoja na kuwawajibisha wwaliopo madarakani. Lakini mazingira wanayofanyia kazi si rafiki. Wanakutana na unyanyasaji kwa sababu tu ya kusaka na kutangaza ukweli. Kipato cha walio wengi sio cha kutegemea na hakikidhi mahitaji yao muhimu.

"Wanahabari wanayo haki ya kulindwa dhidi ya vitisho na unyanyasaji. Wanastahili kuwa na mikataba ya kazi na yenye maslahi mazuri. Sheria ziwalinde wanahabari, badala ya kuwatisha ili wasiibue ukweli. Nafasi ya waandishi wa habari katika jamii ni muhimu; sisi sote tunapaswa kufanya kila tuwezalo kuwalinda na kuwastawisha." Amesema Eyaku

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad