HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 6, 2024

Mikumi `Bambam’

 

Kanga wakiwa katika hifadhi ya Mikumi.Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Agustine Masesa  akizungumza na waandishi habari katika Hifadhi ya Mikumi, Mkoani Morogoro.


*Watanzania wakaribishwa kuitembelea kujionea vivutio lukuki
*Masesa awakaribisha wapendanao kwenda kupendana hifadhini humo

Na Mwandishi wetu
WATANZANIA wameaswa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi kutokana na kuwa vivutio vingi pamoja na kuwa na miundombinu ya Babaraba ya Lami ya kufikika.

Hayo ameyasema Mkuu wa Uhifadhi hiyo Kamishina Msaidizi Uhifadhi Agustine Masesa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Hifadhi ya Mikumi.

Amesema kuwa hifadhi ya Mikumi ndio hifadhi ambayo kila mtanzania anaweza kumudu kwa gharama ya kutembelea ikiwa ni pamoja ya kupata malazi.

Amesema katika kufurahi kwa kiwango cha juu siku ya wapendanao ni kufika Hifadhi ya Mikumi kutokana na upekee wake.

Masesa amesema kuwa katika sikukuu ya wapendanao ambayo hufanyika kila Februari 14 ya kila mwaka kutenga bajeti ya kutembelea Hifadhi ya Mikumi kwani kuna mazingira tulivu na wanyama wa kila aina kuwemo katika hifadhi hiyo

Amesema kuwa idadi ya wanaotembeleaji Mikumi baada ya Filamu ya Royal Toure ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan idadi hiyo imeongezeka kwa kufikia watalii kwa mwaka 2022/2024 watalii 109,012 tofauti na miaka ya nyuma

Aidha amesema Mikumi licha ya kutumia usafiri wa magari pia usafiri wa reli kwa mikoa ya Mbeya wanaweza kufika na hata wageni wa nchi jirani ikiwemo Zambia kutumia reli hiyo.

Mkuu wa Uhifadhi Mikumi Kamishina Msaidizi Uhifadhi Masesa ameongeza kuwa usalama katika hifadhi ni asilimia 100.

Amesema Hifadhi ya Mikumi ni ya kipekee kwa kuwa na wanyama watano Big Five ambao ni Tembo ,Simba ,Nyati ,Chui na Faru.

Amesema barabara za kutembelea katika hifadhi ziko katika hali ya ubora kwa nyakati zote za kutembelea mchana kwa usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad