HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 10, 2024

MALISA: Wasanii Tumieni Hifadhi za Kanda ya Mashariki Kuleta Uhalisia wa Maudhui

Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Mashariki Isaria Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Vivutio vilivyopo katika Hifadhi za  Kanda ya Mashariki.


Baadhi ya wanyama waliopo katika Hifadhi ya Mikumi.


*Wasanii kutumia hifadhi zetu ni kuunga Mkono Filamu ya Royal Toure.

Na Chalila Kibuda,Michuzi
KAMISHNA Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya mashariki Isaria Malisa amewataka wadau amewataka wadau wa michezo hasa ya muziki na filamu kuhakikisha wanatumia maandhari zilizopa Kanda ya Mashariki kutokana na kuwa vivutio vya aina yake na kuleta uhalisia kwa jamii.

Hifadhi zilizo Kanda ya Mashariki zilizopo katika Mikoa ni Mikumi (Morogoro) Saadani (Pwani),Udizungwa (Morogoro) pamoja na Hifadhi ya Nyerere (Pwani).

Malisa amesema kuwa uhalisia kazi zao wakitumia hufadhi ni uzalendo kwa kumuunga Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Filamu yake ya Royal Toure.

Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Malisa ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu fursa zilizopo katika Hifadhi za Taifa ikiwemo Mikumi ambaapo amesema Bado baadhi ya wasanii wanashindwa kutumia hifadhi zetu kwa kuboresha kazi zao badala yake wanalazimika kwenda nchi za jirani kukamilisha maudhui Yao.

Anasema kuna haja ya wasanii kuonesha mfano kwa Jamii hasa kuhamasisha masuala mbalimbali ambayo yamekua yanaleta tija kwa taifa Ili kuwa mfano bora Kwa jamii kwa kuitangaza nchi ya tanzania kupitika utalii katika mitandao ya Kijamii

"Nazungumza hapa ni nyuma yangu kuna kundi la Tembo hivyo mtu akiimba kuhusu Mnyama Tembo anaonekana na ubunifu unakuwa unaonekana"amesema Malisa .

Amesema milango ya kuingia katika hifadhi ziko wazi Kwa wadau wa Sanaa katika kuboresha maudhui hivyo wanaweza kutembelea hifadhi ya mikumi ili kurekodi Maudhui na hifadhi zingine.

Anasema kwa karne hii hakuna haja ya wasanii kusafiri maeneo mbalimbali kufanya kazi zao badala ya kutumia fursa zilizopo ndani yq nchi yetu kutokana na mazingira rafiki katika kuhamasisha utalii.

"Hapa hifadhi ya Mikumi Kuna Viwanja vingi vya michezo unaweza kuandaa bonanza la michezo lifanyike hapa na ukapatiwa kibali baada ya kufuata utaratibu."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad