HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 13, 2024

Jaji Warioba Aeleza Alivyomtuliza Lowassa Baada ya Kukatwa CCM

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema Hayati Edward Lowassa alikuwa kiongozi mwenye hekima na mvumilivu na kwamba hata alipokejeliwa na kuchafuliwa hakurudisha mashambulizi.

Jaji Warioba ametoa kauli hiyo katika shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Edward Lowassa, leo Jumanne,  Februari 13, 2023 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

"Alikuwa ni mtu mwenye imani kwamba ana wajibu wa kulitumikia taifa, alikuwa na maono yake, alikuwa na vipaumbele vyake alionyesha katika utumishi wake, alikuwa mtu wa vitendo. Hakutaka kugombana na watu katika maisha yake, kuna maneno mengi yalisemwa alipata kejeli.

“Alipata matusi lakini hakurudisha hata siku moja alikuwa kiongozi mwenye busara pamoja na mapungufu yake alikuwa na hekima sana," amesema Jaji Warioba.

Katika hatua nyingine, Jaji Warioba ameeleza namna alivyomtuliza Lowassa, katika kipindi kigumu cha kukatwa jina lake kwenye mbio za kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 na kujiuzulu kwake uwaziri mkuu 2008.

"Wakati ambao alikuwa anaona kuna jambo muhimu alikuwa ananitafuta kwa majadiliano , kwanza ilikuwa 1995 yeye na wengine pamoja na Rais mstaafu Jakaya Kikwete anaingia katika kinyang'anyiro cha kugombea urais hakuvuka kamati kuu, alihuzunika sana zaidi aliyetia msumari alikuwa Mwalimu Nyerere, alinitafuta alikuja kwangu Oysterbay akasema ana uchungu na alikuwa anatuhumiwa wakashindwa kumsikiliza wakaamua wakamtoa na bahati mbaya zaidi alichochea Mwalimu." Amesema Jaji Warioba.

Jaji Warioba amesimulia. "Nikamwambia haya ni mambo ya kisiasa usivunjike moyo wewe bado kijana nikamshauru asikae nayo Moyoni aende kwa Mwalimu akamueleza alikwenda wakizungumza pamoja na uchungu ukaisha."

Kuhusu kujiuzulu kwa Lowassa, Jaji Warioba amesema "2008 wakati anajiuzulu uwaziri mkuu alisema hakutendewa haki sababu walimhukumu bila kumsikiliza.

“Mimi nilikuwa Dar es Salaam nikatoa tamko nikasema kama kweli walimtuhumu Waziri Mkuu bila kumsikiliza hawakutenda haki baadae akanifuata nikazungumza naye nikamwambia hayo ni mambo ya siasa hata wangekusikiliza kwa hali ilivyokuwa ilikuwa lazima uachie ngazi."


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad