HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 21, 2024

CHUO KIKUU MZUMBE CHATOA MSAADA WA VITABU VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 103 KWA BODI YA TLSB

Kaimu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Cyriacus Binamungu akikabidhi kitbu kimoja kuwakilisha vitabu 10,535 na vimepokelewa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma za Maktaba, Dkt. Rehema Ndumbaro
 hafla  hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam februari 20, 2024.
Kaimu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Cyriacus Binamungu akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam februari 20, 2024.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma za Maktaba, Dkt. Rehema Ndumbaro akitoa shukrani baada ya Chuo Kikuu Mzumbe kukabidhi vitabu nakala 10,535 jijini Dar es Salaam Februari 20, 2024.
Picha ya Pamoja.

Baadhi ya Wafanyakazi wa  Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya Vitabu kutoka Chuo Kikuu Mzumbe.

CHUO Kikuu Mzumbe wametoa msaada wa vitabu 10,535 vyenye thamani ya shilingi Milioni 103.7 kwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) ikiwa ni mchango wake katika kuhakikisha Maktaba nchini hazikosi vitabu vyenye maarifa mbalimbali kwa ajili ya wananchi kwa ujumla.

Vitabu vilivyotolewa ni vya masomo ya Uongozi, Utawala, Afya, Sheria, Uhasibu, Fedha, Uchumi, Takwimu na Serikali za Mitaa; vitabu ambavyo vimeandikwa na walimu wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Kaimu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Cyriacus Binamungu akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam februari 20, 2024 kwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania -TLSB, amesema kuwa vitabu hivyo vina maudhui yanayoendana na maadili ya Kitanzania.

“Tunawaunga mkono katika utoaji wa huduma za Maktaba kwa ajili ya Watanzania wenzetu ambao wana kiu ya kupata maarifa. Tunafahamu vitabu ni gharama kubwa na ni mchango kwa Watanzania wenzetu ambapo tuna imani hivi vitabu vitakuwa msaada mkubwa kwao hasa ngazi za vyuo na watafiti. Kupitia kwenu, tuna imani vitawafikia wasomaji wengi zaidi.” Amesema Prof. Binamungu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Maktaba, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma za Maktaba, Dkt. Rehema Ndumbaro amekishukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa vitabu hivyo ambavyo watakwenda kugawanya katika maktaba zote za Mikoa na wilaya ili viwafikie Watanzania wengi.

"Kwa vitabu hivi vilivyokuja, naona kila mtu kafurahi kwa sababu wasomaji wetu wanafurahi wakisoma maudhui ambayo yapo katika mazingira yao." Alibainisha Dkt. Rehema.

Ameongeza kuwa bodi ya Maktaba inaendelea kupokea machapisho yote lakini yawe kwenye taratibu, maadili na utamaduni wa Kitanzania.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema katika kutimiza mahitaji ya watumiaji wa Maktaba, sasa wapo katika mpango wa kukamilisha maktaba ya mtandao ili wasomaji wa ndani na nje ya nchi waweze kupata huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad